Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA MPYA YA “HER MOTHER’S DAUGHTER” YAANZA KWA KISHINDO - NI KUHUSU MABINTI WAREMBO MAPACHA. (Episode 1,2,3,4&5)

Baada ya Tamtilia ya My Eternal na Mara Clara kutingisha hisia za wapenzi wa Tamthilia za Kifilipino, sasa hisia mpya sa wapenzi wa Filamu zimeanza kutekwa na Tamthilia mpya ya "Her Mother's Daughter".

Thamthilia hii mpya ya "Her Mother's Daughter" inayoonyeshwa na kituo cha Star TV pamoja na vituo vingine duniani, inahusu wasichana warembo mapacha ambao kupatikana kwao ilikuwa gumzo la familia moja ya kitajiri, ambayo hawakufanikiwa kupata mtoto na hivyo wakaamua kumlipa dada mtu atembee na shameji yake ili awazalie mtoto. Hapo ndipo movie na mapicha picha yalipoanzia.

Dada huyo alifanikiwa kuwa mja mzito wa mapacha wote wa kike, lakini siku zilipozidi kusonga yeye na dada yake ambaye ndiye alitaka mtoto, walishindwa kuelewana kwasababu alijisikia wivu kama shameji mtu kadata kwa dada yake, hivyo yule dada aliamua kuhama katika mji wa Manila na kwenda mbali.Akiwa huko akiishi na baba yake alifanikiwa kujifungua watoto wawili wa kike, yani Celyn na Margaux. Lakini kwa bahati mbaya momoja ambaye ni Margaux, alipotea.

Siku moja Celyn akiwa mdogo aliona picha kwenye gazeti ya mtu mmoja akitangazwa kuwa amefariki, basi Celyn alidhani ni baba yake, kwani alikuwa hamjui. Aling'ang'ana hadi mama yake akampeleka Manila ilikumuaga baba yake. Wakiwa huko waliingia katika soko kubwa la bidhaa mbali mbali, Celyn akishangaa viatu vizuri, alipotea na kuokotwa na mvurana mmoja rika lake aliitwa Ethan, na alimuokoa asingongwa na magari.

Hivyo yule Celyn alikuwa na mama yake mzazi lakini cha kushangaza yule mwingine Margaux aliasiliwa (adopted) na familia ile ya kitajiri ambayo ni ya dada yake aliyeachwa Manila, ambaye pia alikuwa anahitaji mtoto.

Celyn akiwa na mama yake huko kijijini alipokuwa mkubwa alikuwa na ndoto za kuwa mtu wa maana na mwenye uwezo kifedha hivyo kuwasaidia mama na babu yake. Siku moja alifanya mtihani wakujiunga na chuo bila mama yake kujua. Matokeo yalipokuja alikuwa kafaulu kwenda kusoma chuo Manila. Mama yake alimkatalia kata kata, lakini Celyn alitoroka na kwenda chu mjini.

Tayari Celyn amekutana na Ethan amabaye ni bofriend wa pacha wake Margaux ambaye bado hawafahamiani na kwahati nzuri Ethan amemkumbuka Celyn na wanaelekea kuwa marafiki. Lakini Margaux kama anaanza kushtukia urafiki huo.... ni kashe sheshe mpyaaaa.

Fuatilia dondoo za tamthilia hii ya "Her Mother's Daughter" hapa hapa Asili Yetu Tanzania Blog. Karibu sana!!

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.