FILAMU YA WALANG HANGAN (MY ETERNAL) EPISODE YA 66 - SIRI NZITO ZAANZA KUFICHUKA- DANIEL NA KATERINA WARUDIANA.
![]() |
Marco Montenegro na Emily Gidoti |
Daniel anaondoka hadi kwa mama yake Katarina na kumuulizia,
lakini mama yake hakumficha ukweli, kwani alimpasulia kuwa, Nathan na Katerina
wamekwenda air pot wakielekea Marekani.
Daniel bila kupoteza muda aliwasha gari na kuelekea moja kwa
moja air pot, lakini akiwa njiani alijaribu kumpigia Katerina, lakini Nathan
aliinyakua simu na kuizima na kuitupa. Daniel hakukata taama kwani aliwasili
air pot na kumkuta James akiwa tayari amekwisha muandalia passport, hivyo
aliingia ndani moja kwa moja.
Ghafla Daniel alimuona Katerina na kumuita, wote waligeuka
kwa taharuki nyusoni mwao, kwani hakuna hata mmoja ambaye alitegemea kumuona
Daniel pale. Daniel alimsihi Katerina asiondoke na Nathan kwani kesi yake
imekwisha.
Nathan anarukia mazungumzo yao na kumtaka Katarina waondoke huku akisema
“Katerina ni mke wangu wa ndoa”, lakini ghafla Johanna alitinga ndani ya mjengo
na kumsihi Katerina asiondoke na Nathan, kwani ndoa ya Nathan ni batili.
Kusikia usemi huo Katerina anapigwa na bumbu wazi kwani
hakuwahi kusikia swala hilo,
kuwa ndoa yake na Nathan ilikuwa ni batili, ikiwa ni baada ya kibali cha
mchungaji cha kufungisha ndoa kucheleweshwa kukilipia upya.
Nathan anakasirika na kuanza kupasua vyombo ndani, Johanna
anampigia simu baba yake na kumtaka aje haraka. Lakini Marco Montenegro na mama
yake Margaret walipofika, siri ikavuja kwani Marco hakujua kuwa ndoa hiyo
ilikuwa batili.
Miguel anatoroka jela na kurudi uraiani, sasa anapanga njama
za kumuua Marco Montenegro ili amchukue Emily Gidot. Thomas nae anamkaba Nathan
baada ya kujua kuwa ndoa yao
ilikuwa ni batili.
Miguel anampigia simu Margaret na kumpa vitisho kwasababu
ameshindwa kuwasambaratisha Emily na Marco. Margaret anampigia simu Ms Ihenya
na kumueleza ukweli. Je Miguel mtu hatari sana
atamuua Marco Montenegro? Je Daniel atadhurika tena? Nathan je ataamua nini juu
ya Daniel na Katerina? Karibu kwa Dondoo nyingine hapa Asili Yetu Tanzania
(The Best Swahili Blog)
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA