CHRISTINA SHUSHO, UPENDO NKONE NA UPENDO KIRAHIRO, WAKO NCHINI MAREKANI NA CANADA KUTOA HUDUMA.
Kupitia Ukurasa wa kipindi cha Luninga cha "Mwangaza" nimekutana na ujumbe mzuri wa kiroho unaowahusu waimbaji wa Injiri yani Christina Shusho, "Upendo Nkone na Upendo Kirahiro"..ENDELEA.....
Katika kipindi chetu wiki hii tumekuwa na habari za Mwimbaji Christina Shusho ambaye hatimaye harakati za wadau mbalimbali za kumpigia kampeni apate tuzo za Muziki za Kikristo zimezaa matunda baada ya Mwanamuziki huyo, Christina Shusho kufanikiwa Kutwaa Tuzo inayowahusu Wanamuziki wa Injili kutoka Africa ijulikanayo kama Africa Gospel Music Awards.

Itakuwa ni mara ya pili sasa kwa Christina Shusho kutwaa Tuzo kubwa
ambapo mwanzoni mwa Mwezi July 2013 alipewa Tuzo nyingine nchini Kenya
kwenye Tuzo za Groove Awards zinazofanyika nchini humo. Taarifa
tulizozipata kutoka Uingereza zinasema Christina shusho amepata Tuzo
hiyo akishindanishwa na Wanamuziki 6 Kutoka Kenya, Wawili Kutoka Uganda
na Kutoka Tanzania alikuwapo Martha Mwaipaja, yeye kuibuka kidedea.
Kipindi cha Mwangaza kinampongeza sana Christina na pia tunaungana
na Wadau mbalimbali waliompigia debe na hivyo kusaidia kumfikisha hapo
alipo. Kila Lakheri Christina.
Aidha Tunazo Habari kwamba Waimbaji Upendo Nkone, Upendo Kirahilo
na Christina Shusho wako nchini Marekani kufanya Tamasha kwa mwaliko wa
Makanisa ya huko, na Mwangaza ilifanya mazungumzo na Christina kupitia
mitandao na haya ndio yalikuwa majibu ya Shusho nilipozungumza naye..
'Ndio niko USA. Mimi na upendo kilahiro baada ya kumaliza tour yetu
Canada ndio tumeingua hapa USA jana. Tukiwa hapa tunategemea kuhudumu
zaidi ya state kumi ikuwemo Texas, California, Alabama, Ohio, Missouri,
Washington D.C., new york city, n.k
Twaitaji maombi yenu'

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA