MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI ARUSHA, MWAKILISHI WA PAPA ANUSULIKA.
Habari
zilizopatikana hivi punde zinaeleza kuwa kumetokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa bomu katika Parokia mpya ya OLasiti
katika jimbo kuu la Arusha.
Inaelezwa
na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo lililotokea saa tano kasoro
asubuhi kuwa watu kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa hospitali kupata
matibabu.
kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mpaka sasa hakuna mtu aliyepoteza maisha kufuatia tukio hilo.
"Mlipuko umetokea vyombo vya usalama vipo hapa kufanya uchunguzi ,siwezi kukupa idadi ya majeruhi kwa sasa ,ninachoweza kukuambia hakuna mtu aliyepoteza maisha na Balozi wa Vatican yu salama"alisema Sabas kwa njia ya simu.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa bomu hilo lilirushwa na watu waliofika karibu na kanisa hilo wakivalia nguo za kuficha nyuso wakiwa katika gari ambayo namba zake hazikuweza kufamika na kurusha kitu ambacho kililipuka karibu na meza ya misa takatifu.

Misa hiyo
ilikuwa inaendeshwa na Balozi wa Papa nchini Tanzania .
Watu kadhaa wamejeruhiwa ibaya katika ibada hiyo.
Hakuna taarifa
za kifo iliyothibitishwa na mamamlaka za
za usalama bado.
Maafisa wa jeshi la polisi ,askari wa jeshi la wananchi kikosi cha mabomu wapo katika eneo la tukio.

Tutaendelea
kuwahabarisha kile kinachotokea
Habari na NGEREZA

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA