Header Ads

Breaking News
recent

TAMTHILIA YA “MARA CLARA” - "MARA" ANUSURIKA KIFO KATIKA "EPISODE" YA 43 LENITTA ASADIKIKA KUFARIKI.

 Katika mwendelezo wa Tamthilia ya Mara Clara, watazamaji  wote walifahamu kuwa muigizaji Mara kafariki katika Epsod 43 lakini ghafla Mara anaonekana, kumbe aliye fariki hakuwa yeye.

MARA

Mara anajikuta yuko katika  familia ngeni ambayo haijui, lakini pia anajifanya amepoteza kumbu kumbu, lakini kule kwao Clara anazidi kuongeza mazoea ya kutaka atumie muda mwingi na mama yake wa zamani lakini bado ni vigumu.
Amanthe alimtuma mtu ili amfuatilie Gurlly lakini mbini hizo zimetibuka baada ya Gurlly kushtukia mbinu hizo na kumbana mtu Yule na kuweka siri wazi kuwa alitumwa na Amanthe kumfuatilia.
Gurlly anamfuata Amanthe nyumbani kwake na kumueleza kuhusu mtu aliye muagiza amfuatilie, wote wanaghadhabika na kuzichapa mbele ya Avira.
Mama yake Gurlly ameanza kuwa na wasiwasi na mwanae kuwa kuna siri nzito wamemficha kati yake na Clara na anadai kama itakuwa kweli basi hajui maamuzi atakayo chukua. Huko nyumbani  kwa Amanthe kumewaka moto anadai lazima ampate muuwaji wa mwanae.
Japokuwa Clara na Gurly (Baba yake) waliweka agano na siri nzito ya kuzidi kummaliza Amanthe (Baba yake Mara) na kumtaifisha Avira, sasa mambo yaanza kuvuja wazi wazi baada ya makachero wa polisi kumfuata Clara wakitaka aongozane nao ili akafanyiwe mahojiano.

Gurly anawazuia  lakini Clara anapaza sauti kuwa “hapana nitaongozana nao na nitawaeleza yote bila kuwaficha” baba yake anabaki ameduwaa, kwani Clara tayari amekwisha shtukia kuwa baba yake ndiye aliyehusika na mauaji ya “Mara”.
Wameongozana yeye na baba yake pamoja na polisi hadi kituoni, Clara amefunguka kuhusu walivyotekwa na mwanamke aliyekuwa akimpiga mara kwa mara kule walikotekwa.
Clara azidi kujiwa na taswira zinazoashiria baba yake kuhusika katika kifo cha Mara, anambana baba yake naye anakiri kumuuwa Mara.
Siri nzito inazidi kuvuja kwani Gurlly  awapigia simu maaskari na kuwachongea wenzake, wote wauwawa na kubakia mmoja ambaye amebanwa huku Gurlly akimuahidi pesa ili asimtaje , sasa kibao chamgeukia  Christina kuwa ndiye aliyefanya mpango wote wa mauwaji.
Kule nyumbani mama yake Gurlly anaingia chumbani kwa Gurlly na kupekua box na kupigwa na butwaa, kwani lilikuwa limejaa pesa.
Nini kitaendelea, tazama Star TV na karibu tena kwa dondoo  nyingine za tamthilia hii hapa hapa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.