Header Ads

Breaking News
recent

GIDABUDAY (MRATIBU - SOKOINE MIN MARATHON) AELEZA HISIA NA SHUKURANI ZAKE KWA RAIS, WAZIRI WA HABARI UTAMADUNI NA MICHEZO, NAMELOK SOKOINE NA WADAU WOTE.

Baada ya tukio la kihistoria kuwekwa na mwanariadha wa zamani na mwanaharakati wa mchezo wa riadha nchini maarufu kama Wilhelm Gidabuday, yeye kama mratibu wa mashindano ya kumbu kumbu ya "Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013" yaliyofanyika 12/4/2013 huko Monduli, sasa aelezea kwa kina hisia zake kuhusu tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Gidabuday amemshukuru sana Mh. Dr. Jakaya Kikwete, kwa kutambua umuhimu na uwepo wa siku ya kumbu kumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki mnamo 12/4/1984 kwa ajali ya gari.

Pia pamoja na kummwagia shukurani za dhati Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Dr. Fenella Mukangara, amemuomba Mh.Rais Kikwete kumuunga mkono wakati bado akiwa madarakani katika harakati  alizoanzisha za kukusanya nguvu ili kujenga kituo cha michezo cha kitaifa hapa nchini.

Gidabuday (kulia) akiwa na mwanariadha wa kimataifa "Phaustin Baha" wakiwa makini kuhakikisha zoezi la utoaji vyeti kwa washindi wa riadha unafanikiwa.
Gidabuday aliyesimamia kidete kuanzisha mbio za "Edward Moringe Sokoine Mini Marathon 2013" ambayo sasa imeungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete aliyeahidi kwa mwaka kesho kuwa mgeni rasmi katika full Marathon ya kumuenzi hayati Edward Moringe Sokoine katika kutimiza miaka 30 tokea afariki tarehe 12/4/1984 na kuzikwa kwake Monduli, Gidabuday amewashukuru viongozi woote wa kitaifa waliohudhuria pamoja viongozi wote wa riadha mkoa waliojumuika nae kukamilisha tukio hilo.

MSIKILIZE AKIELEZA HISIA, CHANGAMOTO NA SHUKURANI ZAKE.


Pamoja na shukurani zote kwa washiriki wote wa kumbu kumbu za Edward Sokoine, Gidabuday ameishukuru familia ya hayati Edward Sokoine, pia Mh. Namelok Sokoine kwa kushirikiana nae kwa karibu katika kukamilisha mchakato huo. Mwisho kabisa ametoa shukurani zake za dhati  kwa ushirikiano wao wa karibu na wadhati kutoka kwa WAZALENDO 25 BLOG na ASILI YETU TANZANIA BLOG.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.