TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE YA 46 – WAZAZI WA MARA WAGHUBIKWA NA WASI WASI, WAENDA KUUFANYIA MWILI VIPIMO VYA DNA.
![]() |
| "CLARA" |
Clara anaachwa nyumbani na bibi yake, akimuhudumia lakini
Clara anaonekana kukereka sana na bibi yake. Clara anamuacha na kwenda kwa mama
yake wa zamani – Alvira.
Tayari Mara amerejea na kumkuta bibi yake akiwa ameachwa
mwenyewe ndani, amuelezea jinsi alivyookolewa, lakini Mara na Christiani
wanafanikiwa kuondoka kabla ya Garl kurudi.
Amante aenda anaamua kenda kwa Garl kwa siri ili kufanya
uchunguzi wa kile kiatu kimoja polisi walichokikuta baada ya kurushiana risasi
na Garl. Amante anafika kwa Garl na kumkuta Yule bibi mwenyewe na kumuambia
kuwa Garl anahusika katika kifo cha mwanae.
Pia anafanikiwa kukiona kile kiatu, ghafla Garl anafika na
kuanza kupigana na Amante. Huku kule Christian aendelea kumficha “Mara”.
Kwa upande wa Clara anang’ang’aniza kurudi kwao yani kwa
Alvira. Clara hapendi kumuhudumia bibi yake na sasa amebeba mizigo yake na
kurudi nyumbani na Alvira amempokea ikiwa ni mara ya pili baada ya Suzan
kufuata huko.
Mara na Christian wanaenda kumuona bibi yao lakini wakiwa
bado ndani Garl anaingia lakini wanafanikiwa kuondoka, nakumuacha Garl akimsaka
Clara.
Wanaamua kumfuata huko lakini Clara amewakana mbele ya Alvira na Amente
na kumwambia Suzan kuwa “sikupendi kwasababu wewe si mama yangu” Garl aamua
kupiga kimia na kumchukua Suzan hadi nyumbani.
Mama yake Christian amkuta MARA chumbani na kushikwa na uoga
kama aliyeona mzuka uliofufuka. Anamuita Christian na kumueleza kuwa amemuona
MARA, lakini Christian anapotezea kama vile ni ndoto. Kule kwao Clara kahamia
kabisaa kana kwamba ndo kwao. Mama yake Christian ampigia simu Clara na
kumueleza kuwa amemuona Mara kwake.
Mama yake Lenita anafika polisi na picha ya mwanae akimtafuta,
kwa bahati Alvira na Clara walikuwa pale wanashikwa na butwaa, hisia zinaanza
kuwajia kuwa huenda MARA alipona katika bomu. Wanaamua kwenda kuufanyia ule
mwili walio uzika vipimo vya DNA.
Clara aamua kwenda kwa Kina Christian ili kufanya uchunguzi
kama kweli “Mara” yungali hai? Huku Mara na Christian wakiwa tayari kuhamia
katika eneo linguine. Je Clara atafanikiwa kukutana uso kwa uso na MARA?
Huku Garl aungana na wenzake na kuingia kwa kina Amante na
kuripua bomu ili kupoteza muelekeo wa ushahidi.
Je nini kitaendelea. Tazama Star TV na karibu tena kwa
dondoo nyingine za tamthilia hii hapa
hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA