MASHABIKI WA TAMTHILIA YA “MARA CLARA” EPISODE YA 45 – MARA AREJEA NYUMBANI WAONANA NA GERLLY NINI KITATOKE?
Mama yake Gurlly amegundua mchezo wa Gurlly kumficha
Christina pamoja na pesa nyingi alizoziona chini ya kitanda,bibi huyo ameamua
kumfuatilia hadi alikomficha na kumuona Christina kwa macho yake.
Gurlly anasutwa na mama yake huku akimpangusa
makofi mawili mashavuni, Gurlly kwa kushindwa kujizuia inabidi akubali kuwa
ndiye aliyemuua “Mara” na anasema lazima ampate Avira kwasababu niwake tu,
lazima wawe pamoja.
Kule kijijini Chistian azidi kumpa kampani ya kutosha Mara,
japokuwa Mara anasisitiza warudi nyumbani kwao mjini. Kwa upande wa Amanthe
wanahisa wa kampuni yake wanazidi kumbana kwasababu alitumia pesa nyingi bila
ridhaa ya kampuni, na yote haya yanadhaminiwa na Christina ili kutupilia jela
Amanth.
Mama yake Gurlly agoma kula na anadai ukweli aliouficha
mwanae ndio utakao muuwa, bibi huyo anamkomalia Clara na kumlaumu huku
akionekana kulia mda wote.
Amanthe anafuata na polisi na kupelekwa katika mahojiano kwa
kufuja shilingi milioni 40, waandishi wanamsonga Amanthe na kumhoji. TV pia
inatangaza kuwa aliyeandaa mbinu za kumuuwa Mara ni Christina.
Amanthe anampigia simu Christina na kumuomba wakutane ili
waweze kuyazungumza, lakini Christina anamwambia kuwa muda ukifika wataonana
lakini sasa haiwezekani.
Bibi huyo anamua kwenda kwa Amanthe na kuonekana kunajambo
anataka kumuambia, lakini kabla hajafanya hivo, anaanguka chini na kupoteza
fahamu, anakimbizwa hospitali, kumbe anaugonjwa wa kupooza. Gerlly anapigiwa simu, wanakutana na Amanthe,
Gerlly anamtwisha ngumi.
Gurll anakwenda nyumbani kuchukua pesa ili akalipe
hospitali, lakini anakutana na box tupu alipokuwa ameziweka hazipo, anamkalipia
Suzan akimuuliza ni nani amechukuwa pesa zake. Anataka kumpa kichapo,
Clara anamsaidia Suzan asipigwe.
Avira anaenda kumtembelea mama yake hospital, hawezi kuonge
lakini anang’ang’ana kumueleza kitu lakini kabla Avira hajatambua kitu
chochote, Gurlly anaingia na kutoa Avira inje.
Gurlly anadai ili amhamishe Christina kule aliko inabidi
ampatie pesa. Christina anamuagiza aende kwake achukue pesa na vitu vya thamani
ili aweze kumuhamisha. Lakini baada ya Garlly kuingia ndani tu gari la polisi
likatia tim pale na kugundua kunamtu ndani. Wanaamua kuingia na kuanza
kurushiana risasi, Gerlly anapata nafasi ya kutoroka huku akiwa amepigwa
risasi.
Huko kijijini Mara anawasi wasi sana, anataka kurudi
nyumbani lakini Christian anamzuia kwasababu huko hali bado si shwari.
Christian na Mara waanza safari ya kurejea nyumbani. Wakati Mara na Christian wanafika kumuona bibi yake
wote wakiwa ndani, huko nje Gurlly anawasili. Je nini kitatokea? Au Gurlly
ataamua kumteka Mara tena au?
Nini kitaendelea, tazama Star TV na karibu tena kwa
dondoo nyingine za tamthilia hii hapa
hapa.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA