UKWELI KUHUSU VYAKULA KATIKA DINI YA KIKRISTO.
Nimekuwa nikisikia malumbano kadha wakadha mafundisho mbali
mbali katika masuala ya vyakula, lakini hayo yote hutokana na mgawanyiko wa
imani za watu mbali mbali wa dunia hii.
Lakini ni vyema wapendwa katika Kristo Bwana wetu wakarejea
katika maandiko matakatifu na kuweza kuyatumia ipasavyo bila kujichanganya. Na
nukuu vifungu hivi kutoka katika Biblia Takatifu;
"Basi Roho anena wazi wazi ya kwamba nyakati za mwisho
wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya
mashetani, kwa unafiki wa watu wasemao
uongo, wakichomwa moto dhamiri zao wenyewe; wakiwazuia watu wasioe, na kuwaamuru
wajiepushe na vyakula, ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio
na imani wenye kuijua hiyo kweli.
Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni
kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwakuwa
kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba” (1Timotheo 4: 1-5)
“Vitu vyote ni halali, bali si
vitu vyote vifaavyo. Vitu vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo. Mtu
asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. Kila kitu kiuzwacho sokoni
kuleni, bila kuuliza – uliza, kwaajili ya dhamiri; maana Dunia ni mali ya Bwana
na vyote viijazavyo.
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni
kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza – uliza, kwaajili ya dhamiri.
Lakini mtu akiwaambia, kitu hiki kimetolewa sadaka, msile, kwa ajili yake yeye
aliyeonyesha, na kwa ajili ya dhamiri.” (1Wakorintho
10:23 – 28)
.
.
MWENDELEZO WA NUKUU ZA BIBLIA ZINAZOLENGA KUJENGA JAMII YETU,
ZITAKUJIA ZAIDI HAPA HAPA.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA