UKATILI WA POLISI KUMFUNGA DEREVA TAX NYUMA YA GARI NA KUMBURUZA NCHINI AFRIKA KUSINI SASA WAFANYIWA UCHUNGUZI.
Kamati maalumu ya kuangalia
shughuli za polisi huko Afrika kusini inachunguza kisa ambacho dereva
mmoja wa Taxi raia wa Msumbiji alifungwa nyuma ya gari la polisi na
kuburutwa katika barabara za mji wa Johannesburg.
Dereva huyo aliripotiwa kufariki baadaye wakati alippokuwa kizuizini. Shirika la Amnesty International limesema kuwa picha hiyo ni dhihirisho la hofu ambayo wamekuwa nao kwamba visa vya ukatili wa polisi vinazidi kuongezeka nchini Afrika kusini.
Msemaji wa polisi alisema alishtishwa na kisa hicho.
Vyombo vya habari vilisema kuwa polisi walimtendea ukatili dereva huyo baada ya kumtuhumu kwa kuegesha gari lake visivyo, mashariki mwa Johannesburg.
Chanzo: BBC SWAHILI
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA