ZOEZI LA UTOAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA LAZINDULIWA RASMI LEO NA RAIS KIKWETE.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete leo amezindua rasmi zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa katika
sherehe zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Sherehe
hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali wakiwemo marais
wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Amani Abeid Karume. Baada ya
zoezi la uzinduzi, Rais Kikwete aliwakabidhi baadhi ya viongozi vitambulisho
vyao vya taifa.
Rais Kikwete akimkabidhi kitambulisho rais mstaafu wa awamu
ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Akimkabidhi kitambulisho rais wa awamu ya tatu, Benjamin
Mkapa.
Wasanii mbalimbali wakiongozwa na Muumin Mwijuma (wa pili
kushoto) na Isha Mashauzi (wa pili kulia) kutoa burudani wakati wa sherehe
hizo.
Wasanii kutoka THT wakiongozwa na Linah Sanga (kulia)
wakizikonga nyoyo za wageni waliohudhuria zoezi hilo.
(PICHA NA MAKONGORO OGING' / GPL)
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA