Header Ads

Breaking News
recent

PRECISION AIR YAZINDUA SAFARI ZA KIGOMA


· Sasa wateja wake kulipa Sh 199,000 kwa kila safari kutoka Dar hadi Kigoma kila siku
· Safari zote kufanyika mapema kabla ya safari za treni kutoka stesheni ya Dar es Salaam
. Sasa idadi ya safari za shirika letu zafikia 19

DAR ES SALAAM, JANUARI 31, 2013 – SHIRIKA la ndege la Precision Air (PW) limezindua safari zake za kila siku kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kupitia Kigoma Airport kwa kutumia ndege yake aina ya ATR 42 na hivyo kufanya idadi ya safari za shirika hilo kwenye soko kufikia 19.
Uzinduzi wa safari za Kigoma utawezesha shirika hilo kufanya safari zake kila siku kwenda Kigoma kwa kutumia ndege yake aina ya ATR 42-600. Maendeleo haya yanakuja miezi michache baada ya uzinduzi wa safari mpya mkoani Mbeya.

Ndege hiyo itakayofanya safari za kila siku kwa kutumia dakika 60 kwa kupitia Mwanza. Wakati safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma kupitia Mwanza zitafanyika siku za Jumatatu, Jumatano Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 12 asubuhi na kufika Mwanza saa 7.30 asubuhi na kuunganisha Kigoma saa 4 asubuhi ya siku hiyo na kufika Kigoma saa 11.10 asubuhi.

Kuondoka Kigoma kwa siku hiyo itakuwa ni kuanzia saa 11.40 asubuhi na kufika Mwanza saa 12.50 mchana na kuunganisha Dar es Salaam saa 13.00 mchana na kufika mwisho w safari yake saa 15.00 alasili.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Masoko wa Precision Air, Linda Chiza, alisema kuwa safari hizo mpya zitatoa fursa kwa wafanyabiashara wengi na watalii kuweza kutalii kwenye vivutio mbalimbali vya kitalii mkoani Kigoma.

“Tunayofuraha kuzindua safari hizi za Kigoma na tunaamini kwamba nyongeza hii ya safari ni dhahiri itaweza kuchangia ongezeko la uchumi katika mkoa wa Kigoma,” anaeleza Chiza

Alieleza pia kuwa nauli ya kutoka Dar es Salaam-Kigoma ni kiasi cha Shilingi 349, 000 ikiwa ni safari ya kwenda na kurudi. Huku gharama ya nauli Dar es Salaam kwenda Kigoma pekee ni Shilingi 199,000.

Mkoa wa Kigoma una wastani wa watu takribani milioni 2 ambapo mkoa huo una pakana na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kutokana na hilo, safari hizo za Kigoma zitakuza biashara na kuwanufaisha wafanyabiashara ndani ya nchi na nchi jirani ya DRC. Safari hizo za Kigoma zinatarajiwa kukuza sekta ya utalii nchini.

Kigoma yenye bandari ya Lake Tanganyika ni moja ya bandari zilizogubikwa na shughuli nyingi ambapo kihistoria ilikuwa ndio bandari pekee yenye reli inayounganisha (mji wa Kalemie nchini Kongo), na vilevile kupitia reli hiyo bandari ya mkoa huo inaunganishwa moja kwa moja na bandari ya Dar-es-Salaam kwa ustawi wa mikoa hiyo na watu wake.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.