MSANII WA MUZIKI MAARUFU KAMA 'BUIBUI' AGONGWA NA PIKI PIKI NA KUVUNJIKA MGUU.
Msanii Frank
Ktende a.k.a Buibui, alipata ajali weekend hii, kwa kugongwa na boda boda
maeneo ya Kinondoni studio, na kusababisha mguu wake wa kushoto kuvunjika na mguu
wa kulia kuteguka
Kisa cha mpaka kufikia kugongwa na pikipiki hiyo, ni pale
alipokuwa na washkaji zake na mwanadada mmoja alimtaja kwa jina la Lina J,
ambae ni mschana anaefanya nae video ya wimbo wake, video iliyokuwa inataki kukamilika siku ya jana.
"yule msichana nikamwambia kama vipi huu muda umeenda
sana, mida ya saa saba saa nane, turudi tu home
tukapumzike kwasababu kesho tena tunamalizia hii video,huku na huku
tukaondoka, lakini katika wale vijana tuliokuwanao, mmoja simfaham ila mwingine
namfahamu, sasa huyo mshakaji alikua anamtaka huyo msichana, mi sijawahi
kumtongoza, kwasababu namchukulia kama dada yangu nae ananichukulia kama kaka
yake , na mimi sikupenda kwasababu yule sio malaya, nikaona bora nimrudishe
yeye kwanza halafu na mi ndio nirudi
kulala kinondoni.
kumshusha yule, sasa yule jamaa alikua kakaa mbele akawa kama
amemaindi hivi, kwanini buibui kakubali tumrudishe huyu kwanza, kwanini asituache nae, kwasababu
alikua anafosi wanishushe mi kwanza halafu wao waendelee nae safari yao, sasa
yule dada akaniambia "Buibui, nipeleke mimi kwanza huwezi juwa naweza
nikafanyiwa kitu kibaya" kumrudisha akashuka wakawa wananirudisha mimi
Kinondoni, basi kufika studio mi nikashuka lakini yule jamaa alikua kalewa
akaanza kutoa shit huna lolote, nikashuka, nikawa natembea, sa wakati natembea
kuna mshkaji akanambia mbona huyo jamaa ameshika jiwe kwa nia ya kukupiga, sa
mi nikageuka kuangalia mshkaji gani huyu anaetaka kunipiga, wale wa bajaji
kwasababu wananijua wakamuwahi , sa ile nageuka kushoto kwangu, narudi kuangalia
kulia kwangu, nakutana na pikipiki na moto ikanigonga, lakini nilikua kwenye
service road."
Source Dj Fetty

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA