MASTAA WA FILAMU NA MUZIKI BONGO 'FLORA MVUNGI' NA SHILOLE WAELEZEA KUHUSU UGOMVI WAO.
| FLORA |
| SHILOLE |
Nilizungumza na wasanii juu ya kuwakutanisha wiki hii ili
tufunge ukurasa wa bifu lao lakini majibu yalikuwa ni tofauti kabisa na
matarajio. Nini kilichotokea? Fuatana nami sasa…
Funguka: Shilole habari za tangu wiki jana?
Shilole: Nzuri, naona umeibuka tena.
Funguka: Kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba wiki hii ni
lazima niwakutanishe wewe na Flora. Kabla ya kuendelea, hebu wakumbushe
wasomaji wangu wiki iliyopita ulisemaje nilipotaka kukukutanisha na Flora?
Shilole: Nilisema siwezi kukutana na Flora kwani nina mambo
mengi ya kufanya na kinachonishangaza ni kwamba yeye anachonga kwenye vyombo
vya habari mambo yake ili ionekane mimi ndiye ninamchafua. Siwezi kupoteza muda
wangu kuzungumzia suala la msanii huyo kwani anasaka umaarufu kwa kutumia jina
langu.
Funguka: Kwani wewe na Flora aliyetangulia kuwa na jina
kubwa katika sanaa ni nani?
Shilole: Ni yeye lakini mimi nimekuja nyuma yake na nyota
yangu ya sanaa imeng’aa na kumpita, ndiyo maana sasa anahaha kusaka kurejesha
jina lake kwa kutumia mgongo wangu. Mimi niko juu yake kwani Mungu amefanikisha
kufika hapa nilipo.
Funguka: Mbona siwaelewi, Flora anasema wewe ndiye
ulianzisha ugomvi kwa kuanika kwenye vyombo vya habari kwamba amefulia kisanaa
baada ya kuhamishia penzi lako kwa H. Baba (Hamis Ramadhan). Inavyoonekana
ninyi wote mnachezea akili za Watanzania kwa kujionesha mna bifu kumbe mnakuza
majina yenu kiaina?
Shilole: Siyo kweli. Mimi nina uwezo wa kisanaa hivyo siwezi
kutegemea kutengeneza bifu na msanii mwenzangu kwani kazi zangu zinaniwezesha
kuniweka katika chati nzuri ya muziki wa kizazi kipya na filamu.
Funguka: Sawa, vipi kuhusu suala la kukutana na Flora ili
mmalize tofauti zenu?
Shilole: Siko tayari kukutana na mwanamke huyo, nina mambo
mengi ya kufanya na sasa ninavyoongea na wewe naelekea studio kurekodi ngoma
yangu nyingine. Siwezi kupoteza muda kwa kukaa na dada anayetaka kusafisha
nyota yake kupitia mgongo wangu.
Funguka: Dah! Nikuache uendelee na majukumu yako ngoja
nigeukie kwa Flora, nione kama naye anasema nini juu ya kukutana nawe ili
tufunge mjadala huu.
Shilole: Sawa.
Funguka: (Baada ya muda) Napiga namba yake siipati sijui ana
tatizo gani?
Shilole: Sijui, jaribu kumtafuta shosti wake Baby Madaha
anaweza kukwambia kitu.
Funguka: Kwani naye anahusika na bifu lenu?
Shilole: Ndiyo, naye si alijiingiza mpaka amediriki kusema
mimi natumia madawa ya kulevya.
Funguka: Dah! Ngoja nimtafute.
Shilole: Poa kaka.
Funguka: Baby Madaha habari yako, niambie, nasikia na wewe
umenunua ugomvi wa Shilole na Flora kwa nini umefanya hivyo?
Baby Madaha: Ni kweli, Shilole ni mtoto kwetu,
ikumbukwe kuwa Flora ni wifi yangu kwa
H. Baba hivyo siko tayari kuona anaonewa bila sababu za msingi na lengo lake ni
kutaka kuharibu uchumba wao.
Stori: George Kayala
(Global Publishers)
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA