Header Ads

Breaking News
recent

MADHARA YATOKANAYO NA UKEKETAJI WANAWAKE (FGM)..


Kitendo cha Ukeketaji kwa Wanawake tafiti zinaonesha kwamba ktk nchi za Kiafrika, inakadiriwa kwamba zaidi ya nchi 25 zilikuwa zinaendelea na Mila hii ya kukeketa wanawake.
Hali hii imeonekana pia ktk nchi za Ulaya na Amerika ambapo ilikuwa inakadiriwa zaidi ya Wanawake Millioni 100 walikeketwa, na Vijana wa Kike Millioni 2 walionekana kufanyiwa vitendo hivi kila mwaka, kwa sababu mbalimbali za kidini, ngono, kijamii na usafi kwa mwanamke 

Maana ya Neno Ukeketaji:
 
Ukeketaji ni Kitendo cha Kuondoa au Kukata Kisehemu au Sehemu ya Uke (Kinembe/Kisimi au mashavu) cha Mwanamke kinachofanywa na Mtu/Ngaliba ktk jamii ambaye hajapata mafunzo rasmi, na mara nyingi hutumia vifaa visivyo takaswa na hakuna ganzi yeyote inayotumika.
Kitendo hicho huonekana kama sehemu ya Tohara kwa Wanawake.

Aina mbalimbali za Ukeketaji
 
Kwa ujumla kuna aina tatu (3) za Ukeketaji ambazo zimeonekana kufanywa;
I. Kuondolewa kwa ngozi inayozunguka Kisimi/Kinembe.
II. Kukata sehemu yote ya Kisimi
III. Kuondolewa/kukatwa sehemu yote ya kisimi na Mashavu yote ya uke.

Sababu za Kukeketa:

i. Ni imani za Dini kwa baadhi ya jamii
ii. Ngono – Kuboresha tendo la kujamiana kabla ya ndoa kwa imani ya baadhi ya Makabila.
iii. Kijamii – Kinadhihirisha ujasiri, kupevuka na kwamba sasa anaweza kuolewa ili kuleta heshima ktk familia.
iv. Usafi – Jamii ina imani kwamba Mwanamke asiyekeketwa huwa na Uchafu, hivyo kitendo cha kukeketwa humuweka kuwa msafi na kuonekana kuwa maridadi.

Madhara ya Ukeketaji Wanawake:

Kiafya kuna madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kwa vitendo vya ukeketaji wa wanawake kama;
Ø Kuzimia
Ø Kutokwa na Damu nyingi
Ø Kupata uambukizo (Infection)
Ø Kuambukizwa VVU
Ø Kuambukizwa homa ya manjano (Hepatitis B)
Ø Maumivu makali Kidonda kutopona mapema
Ø Kuoza kwa jeraha
Ø Kupata Tetanus
Ø Maumivu ya Kisaikolojia
Ø Kutofurahia tendo la kujamiana kiufasaha
Ø Maumivu wakati wa kukojoa
Ø Kuziba kwa njia ya mkojo
Ø Kuchanika vibaya wakati wa kujifungua
Ø Kuchelewa kujifungua
Ø Kifo

Wajibu wa Jamii ktk Kupiga Vita Vitendo vya Ukeketaji:
Kukemea na kupiga marufuku vitendo na mila ya ukeketaji wanawake.
Kuelimisha wanajamii kuhusu Athari za Ukeketaji kwa wanawake.
Kuhakikisha sheria inachukuliwa dhidi ya yeyote atakaejihusisha na vitendo hivi vya ukatili.
Kuweka Mkakati endelevu kutoa elimu ktk jamii
Kuwashirikisha Wadau ktk mikutano na habari hususani Viongozi wa dini, serikali, wanasiasa, NGOs mbalimbali za kijamii.

Hitimisho
Ili kupunguza na hatimaye kuwaondolea vijana wa kike katika tatizo ili, kila kiongozi wa serikala, Dini na Mashirika yasiyo ya kiserikali katika ngazi zote anapaswa Kutetea sera za kutokomeza hii mila inayotayarisha majina ya huyu motto wa kike.

1 comment:

  1. Hiyo tamu sana ukija nione nikupe zawadi,ila kuna swali na kwa wale ambao walishakeketwa tuwasaidiaje?

    ReplyDelete

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.