TUSAMEHANE KWA YOTE YALIYOTOKEA KWA MWAKA WA 2012 KWANI SOTE NI BINADAMU TUNAMTEGEMEA MUNGU WA MBINGUNI.
Nichukue nafasi hii adimu na pevu kuandika ujumbe huu kwa ndugu, jamaa na rafiki wote wa ASILI YETU TANZANIA katika kuuaga mwaka wa 2012 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2013.
Hakuna kilicho umbwa kikakamilika bila ya kumtegemea tena Mwenyezi Mungu, matatizo ni sehemu tu ya mtihani tuliowekewa katika maisha yetu. Mimi binafsi namshukuru Mwenyezi Mungu kwa upendo wake anaouonyesha katika maisha yangu siku hadi siku.
Ndugu zangu najua kila mmoja wetu amekutana na changamoto za kimaisha kwa mwaka wa 2012 zenye uzito tofauti tofauti, maana hakuna anayeweza kumpendeza Mungu mwanzo mwisho bali ni kwaimani na toba ndivyo vinatufanya tuendelee kuishi.
Chukuwa nafasi hii kusamehe na kuomba msamaha kwa ndugu, jamaa na mafiki kama uliwakosea kwa namna moja ama nyingine, kwasababu hakuna ajuaye saa wala dakika ya mwisho wa maisha yake. Sahau yote mabaya yaliyokupata kwa mwaka wa 2012 na ufungue ukurasa mpya kwa mengine yaliyo mbele yako.
MWISHO niwashukuru wasomaji wa blog hii, kwani nyie ndio mlionifanya niendelee kuipenda na kusonga mbele katika taaluma yangu ya uandishi wa habari.
ASANTENI WOTE.
ASILI YETU TANZANIA

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA