JENIFER LOPEZ APAGAWA KWA MAPENZI ANAYOPEWA NA DANCER WAKE.
Ni mwimbaji, muigizaji na bonge la performer mwenye miaka 43
lakini bado mrembo kama anamiaka ishirini na kadhaa hivi, mwite Jennifer Lopez
a.k.a J.Lo, ambae amenasa kwenye penzi la dancer wake mwenye umri wa miaka 25
ambae pia ni choreographer wake Casper Smart, amefunguka kuhusu mapenzi
anayopewa na jamaa huyo na kuyaita ni ‘endless love’.
Kauli ya J.Lo imeyabariki mauzo ya jarida moja maarufu
linalozungumzia maisha ya watu mbalimbali, na hii ni baada ya kutoa maelezo ya
kina kuhusu maisha yake yanayohusu boyfriend wake huyo , mitindo anayopendelea
na ambayo hajawahi kuibadilisha, na mapacha wake wenye miaka mine Max na Emme.
“Yuko poa kupita kiasi, ni kama best friend wangu. Naweza
kumwambia kila kitu, ninapojisikia vibaya, na ninapojisikia vizuri. Ananipa
sapoti ya kitabia, mahaba yasiyo na mwisho na sapoti,” alifunguka Jennifer
Lopez.
Jennifer ambae aliwahi kuwa jaji wa mashindano ya American
Idol, alishawahi kuelewa mara tatu na kuachana na masupa star kama P.diddy na
baba mapacha wake Marc Anthony.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA