VIDEO YA WIMBO MPYA WA DIAMOND - 'KESHO' AKIWA NA MWANADADA 'AVRIL' KUTOKA KENYA.
![]() |
| Msanii Diamond akiwa na Avril mwanadada kutoka Kenya. |
Diamond Platnumz, jina ambalo litaendelea kuwaumiza vichwa
watu wengi hasa wasanii wenzake ambao wanaitamani nafasi aliyoshika yeye kwa
sasa, the dude is running this game kwa sasa kiukweli na ni ngumu sana kuamini
kwamba atashuka kiwango soon.
Haujapita muda mrefu since ameachia video kali ya 'Nataka
Kulewa', leo hii anazidi kuwachanganya akili fans wake kwa kudrop another brand
new video "KESHO" ambayo kwa kuitazama tu inaashiria ni ya bajeti na
maandalizi ya kutosha.
This time around Platnumz hajalia kama ilivyokuwa katika
nyimbo zake zilizopita lakini bado yuko kwenye duara la mapenzi, akimwambia
mbaibe wake kuhusu siku ya Kesho ambayo wanapanga kwenda kwa wazazi.
Video hii imefanyika nchini Kenya chini ya Ogopa Videos, na
video girl katika video hiyo ni msanii mkubwa wa kike wa Kenya Avril. Master
Mastar wengine wakubwa wwa Kenya walioonekana kwenye video hiyo ni pamoja na
William Tuva mtangazaji wa Citizen Radio/TV, Collo, na Colonel Mustafa.
Source:Leotainment Tz

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA