SINTAH ARUDI KATIKA UIGIZAJI BAADA YA KUCHEZA FILAMU YA "BIFU".
MWIGIZAJI wa zamani Bongo Christina John ‘Sinta’ amewaambia
wapenzi wa filamu Swahiliwood kuwa yeye ni mkali wa filamu tangu kitambo lakini
alikuwa ametingwa na mambo mengine ikiwa pamoja na masomo sasa karudi na uwezo
wake kauonyesha katika filamu ya Bifu.
“Mimi ni mwigizaji mkongwe na mwenye uwezo katika hilo, nimerudi katika
uigizaji kwa sasa nimeigiza filamu kadhaa lakini katika kuonyesha uwezo wangu
angalia filamu ya Bifu nilivyowafunika wasanii nyota uwezo wangu upo juu katika
kuigiza,”anasema Sinta.
Sinta ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi kiitwacho Harusini
kinachorushwa katika televisheni ya Dtv anasema pamoja kuwa na kazi ya
utangazaji bado si tatizo kwake kuweza kuigiza, huku akifikiria kuwa
mtayarishaji wa filamu katika tasnia ya filamu.
Filamu ya Bifu inasambazwa na kampuni ya kizalendo ya
Papazii Arts Entertainment & Promoters ya jijini Dar es Salaam, katika
filamu ya Bifu imeshirikisha wasanii Farid Kubanda ‘Fid Q’, Mh. Joseph Mbilinyi
‘Mr. Sugu’, Christina John ‘Sinta’ na wasanii wengine nyota katika tasnia ya
filamu.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA