NDOA ZA MASTAA WA BONGO ZILIZOVUNJIKA KWA MWAKA WA 2012.
UWOYANdoa ya staa wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya na mwanasoka wa Rwanda, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ ilikuwa kwenye msukosuko kwa muda mrefu lakini mwaka 2012 ndipo ule uzi uliokuwa umeishikilia ulidaiwa kukatika.
JACK PATRICK
Modo wa Kibongo, Jacqueline Patrick alifunga ndoa ya kifahari na mfanyabiashara Abdulatif Fundikira lakini ndoa hiyo iliripotiwa kuota mbawa baada ya mumewe kutiwa mbaroni kwa msala wa kusafirisha mihadarati ambaye anaendelea kusota nyuma ya nondo za mahabusu katika Gereza la Keko, Dar.
DIDA
Mwaka 2012, mtangazaji mwenye jina kubwa anayekitumikia kituo cha Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, alijikuta akirejea kwenye ukapera baada ya ndoa aliyofunga na mwanaume aitwaye Gervas Mbwiga kuvunjika.
HUSNA MAULID
Mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alifunga ndoa na jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Aboubakar ‘Abuu’. Hata hivyo, ndoa hiyo haikudumu kwani ilivunjika ndani ya muda mfupi.
TITO
Ndoa ya mwigizaji wa filamu Bongo, Yusuf Zimbwe ‘Tito’, aliyofunga na msichana wa mjini aitwaye Pamela Brown iliota mbawa baada ya kutokea songombingo lenye ujazo mkubwa na kusababisha wawili hao kufikishana mahakamani.
SKAINA
Staa wa filamu, Skyner Ally ‘Skaina’ ndiye ambaye ndoa yake na mwanaume aitwaye Saad Omary ilidumu kwa siku chache kuliko nyingine kwani inakadiriwa kuwa na takriban siku nne huku sababu ikielezwa ni kuolewa kwa staa huyo tayari akiwa na mimba ya mwanaume mwingine.
NORA
Pia ndoa ya mwigizaji wa kitambo, Nuru Nassor ‘Nora’ na Masoud Ally ‘Luqman’ nayo ilivunjika. Nora alidai kisa cha ndoa kumshinda ni kutokana na mateso ya ajabu aliyokuwa akikutana nayo hasa kutoka kwa ndugu wa upande wa mwanaume.
Stori: Sifael Paul (Globa Publishers).
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA