Header Ads

Breaking News
recent

MSANII RAY C AMSHUKURU RAIS JAKAYA KIKWETE KWA MSAADA WAKE.

Rehema Chalamila a.k.a Ray C amemshukuru raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kwa msaada wa matibabu yaliyomsaidia kwa kiasi kikubwa kupona maradhi yaliyokuwa yanamsumbua.

 Mwana bongo fleva huyo aliyevuma na jina la ‘kiuno bila mfupa’ pamoja na mama yake mzazi walifunguka wakati wakiwa katika maeneo ya Ikulu ya Tanzania na wakiwa na raisi Jakaya Kikwete wakitoa shukurani zao za dhati face to face. Ray C aliyeooneka akiwa na afya inayoridhisha kwa kulinganisha na hali mbaya ya kiafya aliyokuwa nayo katika siku za hivi karibuni, alimshika mkono J.K na kumshukuru huku akisema yeye ndiye baba yake aliyemponyesha.

Mama yake msanii wa bongofleva Ray C,Mh Raisi wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete,Ray C na Dada yake Ray C wakiwa Ikulu baada ya Ray C kwenda kumtembelea kumshukuru kwa kumsaidia kugharamia matibabu yake maalum ambayo anaendelea nayo mpaka sasa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.