Header Ads

Breaking News
recent

MSANII BEBE COOL KUTOKA UGANDA AMEFUNGUKA KUWA YEYE HATUMII NYAMA YA NGURUWE KAMA UVUMI ULIVYOENEA.


Katika dunia hii kuna vyakula kibao, na kila chakula kinawatumiaji wake hivyo kuchagua vyakula kutokana pia na Imani ya dini zao, Bebe Cool amefunguka kujibu uvumi uliosema kuwa anatumia nyama ya Nguruwe wakati yeye ni Muislam; yeye alijibu..  ''No I'm a Moslem and so I don't eat that thing."

 Bebe Cool amelazimika kuwajibu mashabiki wake katika mtandao wa Facebook baada ya uvumi kuenea kuwa alikutwa amepaki kitu cha Hammer akiwa na mashabiki zake bar pande za Nakulabye ambako ni maarufu kwa kuvinjari na Kiti moto.

Maswali mengi yalizuka na kujiuliza kuwa Bebe Cool alikuwa akifanya nini Pork Joint wakati yeye ni Muislam? Lakini Bebe Cool alikanusha na kusema yeye amekuwa mara kwa mara katika sehemu wanayouza kuku inayoitwa Luwombo, ambako ndipo huwa anahusika sana na siyo sehemu ya kiti moto.

Hatahivyo msanii huyo aliyetamba na wimbo wa "Kasepiki" na huu wa sasa "Kamwako, aliamua kuwatoa wasiwasi mashabiki wake ambao tayari walioonekana kuchukizwa na uvumi huo... alisema
"I want to clear the air by correcting whosoever is saying that I eat pork, No I'm a Moslem and I don't eat that thing. I go to Nakulabye to eat chicken luwombo and to also dine with ma local low end fanz..."

Bebe Cool yuko kwenye hatua za mwisho kuachia video ambao ni zawadi  (Christmas Carol) kwa mashabiki wake wakati huu wa Krismasi.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.