MAAJABU YA DUNIA: NYATI AZAA BINADAMU!!!
KATIKA hali ya kustaajabisha, nyati anayefugwa na raia mmoja
anayeishi nje kidogo ya Jiji la Bangkok nchini Thailand amezaa
kiumbe kinachofanana na binadamu kwa asilimia 80.
Mashuhuda walisema kiumbe hicho kilichozaliwa hivi karibuni,
kuanzia kichwani kwenda hadi tumboni ni mwonekano wa kibinadamu.
Hata hivyo, miguu na mikono yake ina kwato kama
za mama yake ambaye ni nyati lakini kichwani hakuna pembe.
Tangu kusikika kwa tukio hilo, umati kutoka sehemu
mbalimbali za jiji hilo umekuwa ukifika nyumbani kwa mfugaji huyo ambaye
hakutajwa jina kwa lengo la kutaka kushuhudia ‘laivu’ tukio hilo la ajabu na
hivyo kuzua taharuki.
“Kutokana na wingi wa watu kufurika, polisi waliitwa ili
kuhakikisha kunakuwa na amani ya kudumu na watu walitawanywa huku wakisema
mfugaji huyo ndiye pekee anayejua kilichosababisha mnyama huyo kuzaa kiumbe
kinachofanana na binadamu,” alisema shuhuda mmoja. Taarifa zinasema, kiumbe
hicho mara baada ya kuzaliwa hakikuchukua muda mrefu kikafa. Hili ni moja ya
tukio la ajabu linalotajwa kutokea duniani.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA