KAJALA AZIDI KUPATA AFYA GEREZANI
MSANII wa filamu Bongo ambaye yuko nyuma ya nondo Gereza la
Segerea, Dar es Salaam kwa mashitaka ya kuuza nyumba iliyowekewa kizuizi na
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kajala Masanja Ameonekana
kuwa na afya nzuri tofauti na maisha ya gerezani yalivyo.
Kajala aliyepandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, muonekano wake kwa sasa uliwashangaza watu katika mahakama hiyo baada ya kuonekana amenenepa sana kuliko alivyokuwa uraiani.

Kajala aliyepandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu iliyopita, muonekano wake kwa sasa uliwashangaza watu katika mahakama hiyo baada ya kuonekana amenenepa sana kuliko alivyokuwa uraiani.
Baadhi ya watu walisikika wakihojiana wenyewe kwa wenyewe
kama kuishi gerezani kwa muda mrefu kunasababisha mtu kunenepeana kama yeye.
“Hivi kumbe gerezani kunaweza kumnenepesha mtu jamani?
Kajala shavu dodo,” alisema mwanamke mmoja ambaye mwenzake alikuwa kinyume
naye.
Mwenzake: “Ila kunenepa kwa aina hii halafu unakaa kwa muda
mrefu kuna hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Unajua uraiani chakula
kinachukuliwa na kazi za siku nzima, gerezani muda mwingi ni kukaa tu, inabidi
afanye mazoezi ya kupungua.”
Kajala akionekana kanenepa kuliko alivyokuwa uraiani.
Mwingine: “Dah! Hebu mcheki kwanza, yaani anazidi kuwa bomba kila kukicha, sasa
hivi amekuwa shavu dodo kuliko hata alivyokuwa uraiani! Tusidanganyane jamani,
piga ua kutakuwa na mtu anamtunza huyu hukohuko aliko si bure. ”
Hata hivyo, miongoni mwa waliodatishwa na muonekano wa
Kajala ni msanii mwenzake, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’ ambaye alimsogelea na
kutaka kumkumbatia lakini alizuiliwa na askari waliokuwa wakimlinda.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA