FLAVIANA MATATA ACHUKUA TUZO YA "FACE OF AFRICA" KATIKA AFRICAN DIASPORA AWARDS 2012.
Mwanamitindo Flaviana Matata, weekend iliyopita ali update
CV ya mambo ya urembo baada ya kufanikiwa kupata tuzo ya Face Of Africa kupitia
African Diaspora Awards 2012, na kwa sababu hiyo kuzidi kuitangaza Tanzania
kimataifa.Tuzo hizi zilifanyika New-York Marekani jumamosi iliyopita , na lengo
lake kuu ni kuwapongeza wa Africa wanaofanya mambo makubwa nje ya bara hilo.
Flaviana Matata mbali na kujihusisha na urembo pia ana
'Flaviana Matata Foundation' ambayo lengo lake kuu ni kusaidia katika mambo ya
kijamii hasa wasichana, katika jitihada za kuwawezesha kielimu na kupunguza
umasikini.