WAREMBO KUTOKA ULAYA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MISS EAST AFRIKA 2012.
![]() |
|
MISS EAST AFRICA BELGIUM-
Cynthia Ikwene (24).
|
Warembo mbalimbali wanaoishi Ulaya na walioshinda katika
mashindano ya Miss East Africa huko Ulaya pia watashiriki katika mashindano ya
Miss East Africa 2012 yatakayofanyika tarehe 07 Desemba katika ukumbi wa Mlimani City
jijini Dar es salaam
warembo hao ni:
1. MISS EAST AFRICA
BELGIUM- Cynthia Ikwene (24)
2.MISS EAST AFRICA
NETHERLANDS- Mareg Marcos (21)
3.MISS EAST AFRICA FRANCE-
Fiona Ruboneka (24)
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012
zitashirikisha warembo kutoka Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi,
Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion,
Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Mwaka huu yanayosubiliwa kwa hamu yanatarajiwa
kushuhudiwa na mamilioni ya watu Duniani kupitia kwenye luninga zao na pia kwa
njia ya Internet ambapo yatautangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa na
pia kujenga umoja wa Afrika mashariki na kudumisha utamaduni wa ukanda huu wa
Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na
kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA