WAKRISTO NAO WATAKA MACHINJIO YAO, WADAI HUPATA SHIDA.
BAADHI ya wananchi wa Wilaya ya Busega wametaka kuwepo na
machinjio ya Wakristo peke yao kwani hivi sasa
wanapa shida wanapochinja mifugo yao
ambayo wakati mwingine hukamatwa.
Wakitoa maoni kwenye kata mbalimbali juu ya uandikwaji wa Katiba mpya, walisema kutoka na kutokuwepo
kwa machinjio ya Wakristo, baadhi ya maduka ya nyama yamekuwa yakichomwa
kutokana na kudhaniwa yanauza nyama ambazo mifugo yake ilichichwa na Wakristo.
“Katiba ikubali kuwa waumini wachinje wanyama wao, tofauti
na kuwa kwamba machinjio yote yameshikwa na watu wa dini moja tu,” alisema
Iswambula Kiswaga mkazi wa kata ya
Kalemela
Pia alisema kuwa, katiba hiyo ianishe siku ya kufanyika kwa
chaguzi mbalimbali ambapo siku hizo zisiwe zile za kuabudu.
“Uchaguzi uwe unafanyika kati ya siku ya Jumatatu, Jumanne,
Jumatano au Alhamisi jambo analosema litaongeza idadi ya watu wanaopiga kura,
tofauti na sasa ambapo maelfu wanajitokeza kujiandikisha lakini siku ya kupiga
kura ya wanajitokeza wachache.
Naye Enock Kindika, alisema kuwa Rais apunguziwe muda wa
kutawala, awe na vipindi viwili vya miaka
miwili na siyo vipindi viwili vya
miaka mitano.
Anasema kuwa, kwa muda uliopo sasa unawafanya wananchi
wateseke kama walifanya makosa katika
kumchagua kiongozi huyo wa nchi.
Kwa upande wa Musa Simba (18), mkazi wa Kalemela, alisema kuwa idadi ya wabunge
ipunguzwe, na pia kuwafuta wabunge wa kuteuliwa na Viti Maalumu kwa kile
alichosema kazi yao
haionekani.
“Hata vyama vipunguzwe, tuwe na vyama viwili tu
vitakavyoshindana kwenye uchaguzi,” alisema.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA