Treni kubeba abiria 5000 jijini Dar es salaam.
KAMPUNI ya Reli Tanzania(TRL) imesema abiria wanaopata
huduma ya usafiri wa Treni katika Jiji la Dar es Salaam wanafikia idadi ya 5000
kwa kila siku kupitia mizunguko yote miwili.
Akijibu maswali kwa njia ya mtandao Mkurugenzi mtendaji wa
Kampuni hiyo, Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema kila mzunguko mmoja treni
inabeba abiria 300 kwa nauli ya mwanafunzi na mtu mzima ambapo inadaiwa idadi
ya abiria inazidi kuongezeka.
“Kwa kutambua hilo Mikakati ya kuboresha huduma hii ipo
na kuanzia alhamisi ya Novemba 22, mwaka
huu,TRL imeongeza mabehewa mawili zaidi na hivyo kuwa manane kutokana na
ongezeko la abiria wanaosafiri kufikia
zaidi 300 kwa kila mzunguko wa safari”alisema Kisamfu.
Kisamfu aliongeza kuhusu uharibifu wa mabehewa hali hiyo ni
tatizo la usafiri wowote kwa umma ambapo hata Waziri wa Uhukuzi Dk Harrison
Mwakyembe aliwahi kutoa wito akiwataka
Wakazi wa jiji kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa viti na vifaa vingine
katika mabehewa vitendo .
Aliongeza kuwa hata suala la usalama wa abiria ndani ya treni
kila abiria anapaswa kutoa udhirikiano wa kulinda uharibifu kutokana na uhaba
wa askari wanaosimamia usalama katika treni hizo.
“Wito kwa wale abiria wema wawadhibiti wenzao ambao
wanawashuhudia wakitoboa viti na kuvunja vioo kwa vile kila behewa linakuwa na
wastani wa abiria 150 ni vigumu askari mmoja kuwaona hao abiria watukutu
kirahisi bila ya 'kuchongewa na wenzao waadilifu”alisema Kisamfu.
Akizungumzia ukarabati wa mabehewa machakavu yanayoonekana
katika karakana za TRL Kisamfu alise mabehewa hayo hukarabatiwa kutokana na
kiasi cha fedha zikipatikana na kurejeshwa tena katika huduma za reli.
“Kwa mfano katika mradi wa mabehewa 31 ambayo yameanza
kukarabatiwa tokea mwezi Juni mwa huu, 14 kati ya hayo ni ya mradi wa treni ya
jiji na 17 ni kwa ajili ya treni kutoka
Dar kwenda Mwanza”alisema
Kisamfu.
Kuhusu usumbufu unaojitokeza kupitia malipo ya chenji
Kisamfu alisema TRL kwa sasa inajadiliana na Kampuni ya Selcom Wireless
kuboresha huduma ambapo muda sio mrefu
kutawepo utaratibu mpya wa kununua tiketi kwa wingi ambazo abiria ataweza
kuzitumia kwa muda mrefu.
“Endapo Abiria atakutwa na tiketi haina alama ya mashine
atahesabika kuwa amepanda bure na kustahili adhabu kwa mujibu wa taratibu,Hata
hivyo kwa sasa Wakaguzi wanaendelea kukagua tiketi zetu na tahadhari tunayoitoa
kwa wateja kuwa tiketi za huduma hii zinazotumika ni zile zenye tarehe ya siku
husika ”alisema Kisamfu.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA