RAIS BARACK OBAMA AFANYIWA USHIRIKINA.
Kogelo, Kenya
LICHA ya ushindi wa Rais Barack Obama, nyuma ya pazia kuna
taarifa kuwa, mzee mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la
John Dimo (105) alimfanyia mambo ya kishirikina ili kumhakikishia ushindi.
Mganga wa kienyeji aliyefahamika kwa jina la John Dimo
anayedaiwa kumfanyia mambo ya kishirikina Rais Obama ili kumhakikishia ushindi.
Inaelezwa kuwa, siku moja kabla ya matokeo ya uchaguzi mzee
huyo aliingia kwenye kijumba chake cha nyasi kilichopo Magharibi mwa Kenya ambako ni
nyumbani kwa baba wa Obama kisha akafanya ‘mandingo’ yake.
“Baada ya kufanya ushirikina wake, alichukua majumba mawili
ya konokono, moja akalipa jina la Romney na lingine jina la Obama kisha akatoka
nje na kuyatupa mbali.
![]() |
|
Mganga John Dimo akiwa kazini.
|
“Baada ya zoezi hilo,
akayafuata na kukuta lile alilolipa jina la Obama liko mbele ya lile la Romney,
akabaini kuwa ushirikina wake umefanya kazi na ndipo alipowatangazia watu kuwa,
Obama atashinda bila kipingamizi,” alieleza
jirani wa mzee huyo.
Akionyesha ushindi wa Obama.
Hata hivyo, baada ya matokeo kutangazwa Jumatano iliyopita,
mzee huyo alijipatia umaarufu mkubwa na watu waliomfagilia licha ya wengine
kueleza kuwa, ushindi wa Obama umetokana na uchapakazi wake pamoja na kupendwa
na watu na si mambo ya ushirikina.
![]() |
| Rais Obama |





No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA