PAPA MPYA WA COPT ACHAGULIWA MISRI.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Kanisa la Copt la Misri limemchagua papa mpya atayewaongoza
Wakristo wanaokisiwa kuwa milioni-8 nchini Misri.
Papa mpya ni Askofu Tawadros mwenye umri wa miaka 60, na
alikuwa msaidizi wa Papa Shenouda wa tatu ambaye alifariki mwezi wa March baada
ya kuongoza kanisa hilo
kwa miaka 40.
Jina la Askofu Tawadros liliteuliwa na mtoto kati ya majina
matatu yaliyoandikwa kwenye vikaratasi vilivowekwa kwenye jagi.
Uteuzi huo ulitokea katika ibada maalumu iliyofanywa katika
Kanisa la Saint Mark's mjini Cairo.
Mwandishi wa BBC mjini Misri anasema papa mpya ni mtu mwenye
uzoefu mkubwa na maarifa ya uongozi; na kwamba atahitaji sifa hizo katika nchi
ambayo inajadili mchango wa Uislamu baada ya mapinduzi yaliyomtoa madarakani
Rais Hosni Mubarak.
Msemaji wa chama cha Muslim Brotherhood, kinachoongoza
serikali, alinena kuwa wana matumaini kwamba watakuwa na ushirikiano na papa mpya.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA