Header Ads

Breaking News
recent

"NATAKA KULEWA" YA H BABA ANAYODAI KUIBIWA IDEA NA DIAMOND.

Asili Yetu Tanzania.Copyright

H Baba akiwa ameshikilia demo yake ya "Nataka Kulewa ambayo anadai kuibiwa Idea na msanii Diamond baada yakuwa ameachia wimbo wake mpya wa "Nataka kulewa". Diamond aliangusha shoo jana jijini Arusha katika uzinduzi wa jiji la hilo ambapo aliimba pia wimbo wake mpya wa "Nataka kulewa".

H.baba ametuletea (Bongo5) exclusively kipande cha wimbo wake uitwao ‘Nataka Kulewa’ ambao amemshirikisha Q-Chief. Msanii huyo anamshutumu Diamond kuiba wazo na jina la wimbo wake huo katika wimbo wake mpya wenye jina kama hilo. 

JUZI KATI HIVI KUTOKA BONGO 5 

Scandal inayohusiana na wimbo mpya wa Diamond ‘Nataka Kulewa’ imeendelea kuchukua sura mpya baada ya H.Baba leo kuiambia Bongo5 kuwa Diamond Platnumz ameanza kutuma watu wake ili waiibe flash yenye wimbo wake (H baba) ili kusiwepo ushahidi.

“Ninayo kwenye flash lakini siwezi kuiacha sehemu yoyote sababu ameshatengeneza mpaka watu waibe hii flash, yaani sasa ni michongo tu ya ajabu ajabu inaendelea sasa hivi,” amesema.

‘Kwasababu kule studio yaani verse zote zimefutika lakini mimi nilikuwa nayo kwenye flash yaani ile demo nilichukua kwaajili ya kusikiliza nyumbani, studio verse zote zimepotea, huwezi amini.”

Amesema hana lengo la kuuachia wimbo huo lakini atatoa kipande kifupi ili watu wasikie kile anachokisema.
Msanii huyo anasema Diamond alimkuta kwenye studio ya G Records wakifanya wimbo wenye jina hilo (Nataka Kulewa) ambapo Q-Chief aliimba chorus na Diamond kuusifia sana.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.