MSANII AFARIKI GHAFLA....Filamu yake ya mwisho alicheza na AUNT EZEKIEL.
![]() |
| MSANII wa filamu Bongo aliyekuwa akipanda juu kwa kasi, John Maganga (22) amefariki dunia ghafla katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokimbizwa akiwa hoi, inasikitisha sana. |
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, baba mdogo wa John,
Deogratius Shija alisema Ijumaa iliyopita, marehemu alipatwa na maumivu ya
ghafla ya tumbo, akapelekwa Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu ya Mwananyamala, Dar
ambako vipimo vilidai utumbo wa mgonjwa huyo ulitoboka.
![]() |
| JOHN MAGANGA |
Shija: “Daktari akatuambia kutokana na hali hiyo watamfanyia
upasuaji ili kuuziba utumbo huo lakini mara baada ya zoezi hilo daktari akasema
tatizo halikuwa kutoboka kwa utumbo bali kuna kitu kingine.
“Ikabidi tumkimbize Muhimbili ambako madaktari wa pale
walituambia wenzao wa Mwananyamala walikosea kumfanyia upasuaji John kwani
tatizo halikuwa la kufanyiwa upasuaji bali alitakiwa apatiwe dawa.
“Madaktari wakatuambia tumwache pale ili waokoe maisha yake
sisi ndugu turudi asubuhi. Tulipokwenda asubuhi tukaambiwa mgonjwa wetu
alifariki dunia usiku uleule. Imetuuma sana.”
Hivi karibuni, John aliandaa filamu yake ambayo aliipa jina
la Beautfools ambayo yeye alicheza kama mume wa ndoa wa Aunt Ezekiel ambaye
alimtenda John wakati anasoma chuo.
Marehemu alikuwa akienda vizuri katika tasnia ya filamu na
ilisadikiwa angeweza kuziba pengo la marehemu Steven Kanumba. Kifo cha John
kimeacha pigo kubwa Bongo Movies ambayo mpaka leo vilio vimetawala.
Mpaka jana Jumamosi, mazishi ya msanii huyo yalikuwa
yakimsubiri mama yake mzazi aishie London Uingereza.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA