Header Ads

Breaking News
recent

MAAJABU 7 YA DUNIA USIYOFIKIRI KUWA NI MAAJABU.

Kikundi cha wanafunzi darasani walipewa kazi ya kuorozesha 'maajabu saba ya dunia', wanafunzi wote wliwasilisha maajabu saba yao, lakini mmoja wao alionekana kuwa bize kuandika.

Mwalimu akamsogelea na kuuliza kama anatatizo lolote ili amsaidie, msichana huyo alijibu "ninatatizo kidogo". Mwanafunzi huyo aliendelea kusema "nimeshinda kufikilia nikamaliza kwasababu maajabu ni mengi sana!".

Mwalimu akajibu "sawa tuambie uliyoyaorozesha alafu kama kunatatizo tukusaidie". Msichana huyo akasita kwanza, alafu akasema... "maajabu saba niliyoyapata ni haya yafuatayo...

1. KUONA.

Hearing
2. KUSIKIA.
Touch
3. KUGUSA.
Taste
4. KUTOFAUTISHA RADHA.

Feel
5. KUHISI.

Laughter
6.
KUCHEKA.

Love
7. KUPENDA
Drasa zima lilinyamaza kimiaaa kiasikwamba unaweza kusikia mlio wa sindano ikidondoka kwenye sakafu. Vitu tunavyovichukulia kirahisi katika miili yetu na maisha yetu ndivyo maajabu saba ya kwanza.

Mawaidha  - ni kwamba mambo ya thamani zaidi katika maisha hayawezi kujengwa kwa mkono au kununuliwa na mtu.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.