JCB AACHA UJUMBE, YEYE AELEKEA UFARANSA.
Mwanamuziki wa Hip Hop kutokea jiji la Arusha, JCB, ambae aliwahi
kuchukua tuzo ya wimbo bora wa Hip Hop kupitia wimbo wa Ukisikia Paah
katika tuzo za Kilimanjaro Music Awards 2011, amekwenda nchini Ufaransa
kufanya kazi za kisanaa.
Aidha katika mahojiano ambayo bongo5.com imefanya nae (ambayo utayaona hapa chini) JCB ameongelea mengi ambayo anayaona yanazorotesha maendeleo ya muziki wa Hip Hop, kubwa zaidi akizitupia lawama vyombo vya habari upande wa maredio kwa kuwa nyimbo zao (wana Hip hop) hazipewi muda wa kutosha katika playlist za vipindi vyao.
Kwa sasa JCB yupo katika maandalizi ya Album huko Ufaransa akimshirikisha msanii mwingine wa Hip Hop Kindo Man ambaye anaishi Ufaransa.
Angalia Interview ya JCB hapa.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA