G-NAKO: NAKO 2 NAKO BADO IPO HAI, MASHABIKI KAENI TAYARI KUPATA RADHA MPYA.
Hivi karibuni mashabiki wengi wa kundi la Nako 2 Nako
Soldiers la Arusha wamekuwa wakishindwa kuelewa kama kundi hilo limekufa
kutokana na members wake kuwa karibu zaidi na kundi la Weusi.
Akijibu swali kama Nako 2 Nako imeuliwa na Weusi,
G-Nako amesema kundi hilo bado lipo na Weusi si kundi bali ni kampuni ambayo
inajumuisha members watano ambao ni yeye, Lord Eyez, Nikki wa Pili, Joh Makini
na Bonta.
“Chama lipo kama kawaida na soon kinaweza kikanuka kwasababu
imeonekana kuwa kuna mkanganyiko Weusi, Nako 2 Nako, River Camp lakini soon
tutaliclear hili na soon nyimbo ya Nako 2 Nako nafikiri nayo itatoka, alisema G
Warawara.
Aliongeza kuwa walipokuwa pamoja kama Nako 2 Nako walishauriana
kuwa kila mmoja anaweza kufanya kazi yake binafsi nje ya kundi.
Nako 2 Nako Soldiers inaundwa na Lord Eyez, G-Nako na Bou
Nako. Ibra Da Hustler aliyekuwa mmoja wa member wa kundi hilo alijitoa.

Haina mbaya tunasubiria hayo mangoma yenu na yakubali weusiii sanaaa na wata saluti!!!!!lini inatoka!!!
ReplyDelete