Benk Kuu ya Brazil yatakiwa kumuweka Mungu Pembeni yani Kuondoa Maneno haya "PRAISE GOD" katika Noti za Nchi hiyo.
Baadhi yab noti za Brazil
Kiongozi wa mashitaka nchini Brazil Jefferson Aparecido Dias
ameitaka serikali ya nchi hiyo kuilazimisha Benki kuu ya nchi hiyo kuondoa
sentensi inayosomeka ‘God be Praised’ (Mungu asifiwe) kutoka kwenye fedha za
noti za nchi hiyo.
Kiongozi huyo amedai kwamba nchi ya Brazil ni nchi ambayo haiko chini ya dini yoyote
hivyo kuweka sentesi hiyo kwenye noti ni kuvunja haki za watu wengine wasio
wakristo na wasio amini katika dini yoyote ambao wamekuwa wakimpelekea
malalamiko yao kuhusiana na suala hilo.
Kiongozi huyo amesema kuwa, ijapokuwa nchini Brazili watu
wengi ni wakristo lakini kuna maeneo mengine ya nchi hiyo yanakaliwa na watu
wenye imani za Kiislam,Hindu na Budha.
Maandishi katika noti hii yanayomaanisha "MUNGU ASIFIWE".
“kwa mfano hebu fikiria kama noti hizi zingekuwa zina kauli
kama zifuatazo “Asifiwe Allah” Asifiwe Buddha”,Ainuliwe Oxossi,Atukuzwe bwana
Ganesh au “Hakuna Mungu” alisema kiongozi huyo
Kadinali Odilo Scherer, ambae ni askofu mkuu wa Sao Paulo, amejibu kauli
hiyo kupitia akaunti yake ya tweeter kwamba maandishi hayo hayawezi kubadilisha
chochote kwa wasiomuamini Mungu. Lakini yanamaana kwa wale wanaomuamini Mungu,
na kwamba wanaomuamini Mungu pia wanalipia kodi na ndio wengi zaidi hapo Brazil.
"The phrase should make no difference to those who do
not believe in God. But it is meaningful for all those who do believe in God.
And those who believe in God also pay taxes and are most of the
population,"
Ikijibu madai hayo Bank kuu ya Brazil
imesema maneno hayo yaliwekwa kwenye noti za nchi hiyo kwa sababu katiba ya
nchi hiyo inaonesha kuwa serikali ya kidemokrasia ya Brazil iliundwa chini ya ulinzi wa
Mungu, hivyo maneno hayo ni ishara ya uweza wa Mungu katika nchi hiyo.
Source:Leotainment


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA