WALIOFANYA VURUGU ZA KUCHOMA MAKANISA JIJINI DAR ES SALAAM WAFIKISHWA MAHAKAMANI.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
| Baadhi ya washitakiwa wakiingia ndani ya basi la magereza tayari kurudishwa mahabusu ikiwa ni mara baada ya kesi yao kusikilizwa. |
| Washitakiwa kwa pamoja wakiwa ndani ya mahakama. |
Washitakiwa hao waliofikishwa mahakamani hapo wakiwa kwenye
magari matatu ya polisi aina ya Defender majira ya saa 6:26 mchana chini ya
ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamevalia mabomu viunoni, kutokana na kufanya
matukio hayo kama sehemu ya malipizi yao kutokana na madai ya kunajisiwa kwa
mkojo kwa Msahafu kulikofanywa na kijana wa Kikristo.
Baada ya kushushwa, watuhumiwa hao waliamriwa kuchutama
kabla ya kuanza kuingizwa kwenye chumba namba moja cha mahakamani hapo, huku
kukiwa na tahadhari kubwa ya kiusalama ndani na nje ya mahakama hiyo.
Kwa upande wa mashtaka, watuhumiwa hao wamefunguliwa kesi
nne tofauti za jinai kwa mpigo, kesi ya kwanza ni jinai Namba. 240/2012, namba
241/2012, namba 242/2012 na 243/2012.
Watuhumiwa hao walisomewa mashtaka hayo mbele ya Mahakimu
Wakazi wawili Sundi Fimbo anayesikiliza kesi tatu huku moja ikisikilizwa na
Hakimu Mkazi Bingi Mashabara.
Upande wa Jamhuri kwenye keshi hiyo uliwakilishwa na Wakili
Mwandamizi Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya na Joseph Maugo.
Wakili Kweka alidai katika kesi ya jinai namba 243/2012 inayowakabili
washitakiwa 17 ambao ni Maenga Rwenda,
Hamad Euli, Shego Sheso, Ramadhani Mgule, Mashaka Iman, Kassim Juma Kigoni,
Ibrahim Himu, Hamza Fundi Hamza, Mikidadi
Sadick, Juma Mbegu na Rahimu Boga.
Wengine ni Issa Abdallah, Hamis Kmwaga, Ramadhani Mbulu,
Hamed Mohamed, Mohamed Yusuf na Msha Alifa, wanakabiliwa na kosa la kula njama
kutenda kosa la unyang’anyi wa kutumia
silaha kinyume na kifungu cha 287A cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka
2012.
Wakili Kweka alidai kuwa Oktoba 12, mwaka huu huko Mbagala wajatwa waliiba vitu
mbalimbali ikiwamo 'Laptop', 'Printer Projector', spika, saa za ukutani na viti
vya plastiki vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 20 mali ya Kanisa la
Kiinjili la Kilutheli Usharika wa
Mbagala.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, kabla ya kuiiba watuhumiwa
wamtishia mlinzi Michael Samwel kwa mashoka na nondo kwa lengo la kujipatia
vitu hivyo.
Kweka alidai shitaka jingini ni la kuchoma kanisa kinyume na
kifungu cha 319(a) cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ambapo washitakiwa hao kwania
ovu walichoma kanisa hilo mali na kuongeza kuwa shitaka jingine ni la kuharibu
mali kama madirisha, meza, mfumo wa umeme, milango, aircondition vyote mali ya
kanisa hilo ambavyo vyote vikiwa na thamani ya sh 500,000,000.
Wakato huo huo, Naye mtoto aliyesababisha vurugu hizo ambaye
ni mwanafunzi wa Shule ya Chamazi-Machimbo Mbagala, alifikishwa katika Mahakama
ya Watoto mbele ya Hakimu Mkazi Devota
Kisoka akikabiliwa na kosa moja la
kuidhalilisha dini ya Kiislamu kwa
kukikojolea kitabu Qur an Oktoba 10.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA