JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM LAMKAMATA SHEIKH PONDA ISSA PONDA KWA MAKOSA MBALI MBALI YA KUCHOCHEA VURUGU NA UVUNJAJI WA AMANI JIJINI DAR ES SALAAM.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
|
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman
Kova akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
|
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtia
mbaroni Katibu wa Jumuiya tajwa hapo juu maarufu kama PONDA ISSA PONDA kwa
makosa mbali mbali ya kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani jijini Dar es
Salaam.
Aidha hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda aliongoza kundi
la wafuasi wake na kuvamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe
katika Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA ambayo ipo chini ya
Kurugenzi ya Kampuni hiyo.
Mnamo tarehe 12/10/2012 Ponda Issa Ponda aliwaongoza wafuasi
wake walioteka eneo hilo wakidai kwamba wanakomboa. Mali za Waislamu,
zilizouzwa na BAKWATA, uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba kiwanja hicho kina
hati miliki No. 93773 uliotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na mikataba mbali
mbali ya kuuziana au kubadilishana kati ya BAKWATA na Kampuni tajwa hapo juu.
Pia uongozi wa BAKWATA umeletamashahidi kuthibitisha uhalali
wa kiwanja hicho kumilikiwa na Kampuni tajwa. Hivyo watu wote waliovamia eneo
hilo wakiongozwa na Sheikh Ponda wanakabiliwa na shtaka la kuingia kwa jinai
pamoja na uharibifu wa mali katika eneo hilo.
Sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda tarehe 16/10/2012 saa
4.00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambapo aliletwa na pikipiki.
WATU 38 WAMEKAMATWA
KWA KOSA LA KUINGIA KWA JINAI NA UHARIBIFU
Wakati huo huo
sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda Polisi walifanya operesheni
maalumu ya kuwaondoa wavamizi katika kiwanja tajwa hapo juu kinachomilikiwa na
Kampuni AGRITANZA. Watu wapatao 38 walikutwa katika eneo la kiwanja hicho
ambacho kati ya hao (7) ni wanawake na 31 ni wanaume.
Operesheni hiyo ilifanyika tarehe 17/10/2012 usiku wa manane
kuanzia saa tisa hadi saa kumi na nusu usiku kwa muda wa dakika 90. Katika eneo
hilo vilikutwa vielelzo mbali mbali vikiwemo visu na mapanga na pia nyenzo
mbali mbali za ujenzi, pamoja na vifaa vya ujenzi, vielelezo hivyo
vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi tayari kwa ajili ya ushahidi mahakamani.
SHEIKH PONDA
KUSABABISHA VURUGU NA VITISHO
Katika siku za hivi
karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake chini ya
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwa kufanya maandamano kinyume cha
Taratibu na kuhamasisha umwagaji damu jijini Dar es Salaam na nchini Tanzania
kwa ujumla.
Kwa ujumla Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania
inayoongozwa na Sheikh Ponda haijasajiliwa kisheria lakini wanatihumiwa kwa
uchochezi wa hali ya juu ambapo licha ya kufanya maadamano kinyume na sheria
pia siku ya tarehe 12/10/2012 walisababisha kuvunja kwa makanisa zaidi ya
manane, uharibifu wa magari na wizi au upotevu wa vifaa katika makanisa, yote
hayo yameongozwa na Sheikh Ponda na madhara yake ni makubwa.
Sheikh Ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya
dola pamoja na kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumuwa waliokamatwa
kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa mahakamani waachiwe mara moja kabla siku
saba na kadhalika.
Uchunguzi wa watuhumiwa wote 39 unaendelea na kufikishwa
mahakamani mara baada ya kupitishwa na wakili wa Serikali kuthibitisha
mashitaka.
S.H. KOVA – DCP
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUMU YA POLISI
DAR ES SALAAM

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA