VURUGU ZA MAANDAMANO ZANZIBAR - ASKARI AFARIKI..KAMISHNA WA POLISI "MUSSA ALI MUSSA" AFAFANUA ZAIDI.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said
Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa
kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30
usiku katika eneo la Bububu.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa
Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya
UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh
Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.
Kamishna Mussa
amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu waliofanya
mauaji ya Coplo Saidi Abdulrahaman ili kuwakamata na kuwafikisha Mahakamani kama sheria za nchi zinavyowaelekeza.
Amesema mpaka hivi
sasa watu 10 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbali mbali yaliyotokana na
vurugu za jana na upelelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi wa kutekwa Sheikh
Farid unaendelea.
Ameongeza kuwa
kutekwa kwa Sheikh Farid kunatia mashaka kutokana na mazingira ya kutoweka kwake
kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mdogo wake Said Omar Said ambae alikuwa
dereva wake katika hatua za mwisho maeneo ya Mazizini walipokwenda kununua
umeme.
“Sheikh Farid
alimuamuru Said amuache katika eneo hilo
aende nyumbani kupeleka umeme na wakati huo akaendelea na mazungumzo na watu
wengine walikuwemo ndani ya gari nyengine ndogo ya NOAH ambayo nambari zake
hazijajulikana lakini aliporudi kumchukua hakumkuta” alisema Kamishana Mussa.
Amesema fujo hizo
zilisababisha hasara kubwa kwa Serikali, Chama tawala na wananchi ikiwemo
kuchoma na kuharibumiundo mbinu ya barabara, kuharibu maskani za CCM za Kisonge
na Muembeladu kwa kuzichoma moto baadhi ya magari kuvunjwa vioo na kuvunja duka
la pombe na kuiba mali
iliyokuwemo ndani.
Hata hivyo amedai
hali ya Mji wa Zanzibar kwa sasa ni shwari, wananchi wanaendelea na shughuli
zao kama kawaida na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vikosi vyengine vya
ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha amani inadumu muda wote.
Amewataka wananchi
kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao, na kutoa taarifa za
watu waliohusika na vurugu pamoja na mauaji ya Coplo Said Abdulrahaman.
IMETOLEWA NA
IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
dha! Hali bado tete!
ReplyDelete