UJASILI NI ASILI YA MTU, UKIWANAYO UTAKUWA MFANO MZURI KATIKA JAMII: ASILI YETU BLOG
Asili Yetu © All rights reserved
Kijana mdogo pichani
Nelson Fonangwan (muafrika katikati) mwenye miaka 16 amefanya hivyo.Alikuwa amelala nyumbani
kwao na kuamshwa na kelele za majirani ambao walikuwa wakiunguliwa na nyumba.
Aliamka na kwenda kuangalia nini kinaendelea akakuta nyumba
ya jirani ikiungua na mama mwenye watoto wawili akihangaika kuvunja dirisha
kwenda kumuokoa mtoto wake mdogo Adam mwenye miaka 2.
Mama alivunja dirisha bila mafanikio huku moto ukizidi
kuwaka ndipo Nelson alipokuja akavunja dirisha na kuingia ndani kumuokoa
mtoto.Mama akapiga simu 999 ikaja gari ya zimamoto.
Akisimulia moto ulivyotokea mama wa mtoto anasema alikuwa
ameenda nje kutupa uchafu akiwa amemuacha mwanae mdogo jikoni.Kurudi mlango
ukawa umejifunga na kumbe aliacha fying pan jikoni ikaanza kuungua na baadae
moto kuanza kuwa mkubwa.Alijitahidi kuvunja dirisha na mkono ambao aliumia sana
huku akipiga kelele ndio kijana Nelson kutokea na kumsaidia.
Tukio hili lilitokea nchini Uingereza maeneo ya
Southampton.Kijana Nelson Fonangwan asili yake ni Cameroon lakini yupo huko
kimasomo akisomea health and social care,maths na english.
![]() |
| Nelson Fonangwan |


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA