SOPHIA SIMBA, SHYROSE ILIKUWA NIPATASHIKA KATIKA UCHAGUZI WA (UWT)
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
|
Shy-Rose Bhanji, (Kulia), akionyesha uso wa hasira huku
akitulizwa na mjumbe mwenzake, kufuatia tafrani kati yake na mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wanawake Tanzania UWT), Sophia Simba.
|
![]() |
|
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya CCM, (UWT), Sophia
Simba, wakati akiingia katika ukumbi wa Mipango tayari kwa uchaguzi mkuu wa
Jumuiya hiyo.
|
HALI ya hewa iliyochafuka wakati wa Uchaguzi wa Mwenyekiti
wa UWT, imeeleza kuibua vita mpya kati ya mshindi wa kiti hicho, Sophia
Simba na aliyemuuliza swali la
kichokozi, Shyrose Bhanji.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Shyrose alichukizwa na
kitendo cha watu walioonekana kuwa wafuasi wa Sophia ambao walimzomea kwenye
ukumbi wa mkutano, baada ya yeye kuuliza swali lililotafsiriwa kuwa la
kichokozi.
“Shyrose amesema watu wa Sophia wamemdhalilisha sana kwa kitendo chao cha
kumzomea kiasi cha kutaka kumlazimisha atoke nje, kwa hiyo amesema hakubali na
atapambana kwa sababu yeye ni mwanamke jasiri, asiyeogopa chochote,” alisema
mtoa habari wetu.
Aliongeza: “Unajua ndani ya CCM kumekuwa na makundi makundi,
nadhani Shyrose amesema atapambana kwa kuhisi kwamba Sophia anaweza kutumia
nafasi yake ya uenyekiti wa UWT kumbania Shyrose kwenye harakati mbalimbali
ndani ya chama".
SWALI LA UTATA
Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, swali lililoibua mtafaruku
wote ni lile ambalo Shyrose alimtaka Sophia aseme atawasaidiaje wanawake wa CCM
kwa sababu tangu amekuwa mwenyekiti wa UWT miaka mitano iliyopita, hakuwahi
kuonekana hadharani akifanya kazi za kukisaidia chama hicho.
JIBU LIKAWA HIVI
Chanzo chetu kikasema: “Sophia alijibu kwamba yeye ni mtu wa
serikali, kwa hiyo anafanya kazi zake kwa utulivu tena chini kwa chini, siyo
mbwatukaji. Akaongeza kwamba Shyrose amepewa ubunge wa Afrika Mashariki
juzijuzi, kwa hiyo hawezi kujua kazi zinakwendaje”.
VITA ITAFIKA WAPI?
Kwa mujibu wa chanzo chetu, hali ilikuwa mbaya na bila
busara za aliyekuwa mwenyekiti wa kikao, Profesa Anna Tibaijuka, ‘wapambe’ wa
Sophia wangeweza kumtoa nje Shyrose tena kwa msobemsobe.
Imeelezwa kwamba Tibaijuka alizuia Shyrose kutolewa nje
lakini hakuwa na amani baada ya watu hao kuendelea kumzomea.



No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA