RAIS WA MAURITANIA APIGWA RISASI
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz |
Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, amepelekwa
Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.
Kabla ya kuondoka kuelekea Paris, Rais Abdel Aziz alisema
kwenye hotuba iliyotangazwa kwenye televisheni kutoka hospitali, kwamba
ameshafanyiwa upasuaji ambao ulifanikiwa.
Wakuu walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali
waliokuwa kwenye doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.
Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali Abdel Aziz, ambaye anaonekana na mataifa ya
magharibi kuwa anasimama dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo,
alichaguliwa mwaka wa 2009, mwaka mmoja baada ya kupindua serikali.

No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA