MAGDALENA ROY NDIO MSHINDI ALIYETWAA TAJI LA REDD'S MISS TANZANIA 2012
Asili Yetu Tanzania.Copyright
Mshindi wa Redd's Miss Tanzania Magdalena Roy akionekana katika picha akitabasam.
| Magdalena Roy akipunga mkono kati kati, akiwa na washiriki wenzake. |
MISS Dar City Center ambaye pia alishika nafasi ya pili
katika shindano la Redd’s Miss ilala, Magdalena Roy amefanikiwa kuingia 15 Bora
ya Redd’s Miss Tanzania baada ya usiku wa kuamkia leo kufanikiwa kutwaa taji la
Top Model.
Magdalena anakuwa mshindi wa pili kuingia katika hatua hiyo,
akiungana na Miss Mbulu, Lucye Stephano ambaye wiki iliyopita alitwaa taji la
Miss Photogenic.
Katika shindano la Top Model lililofanyika kwenye hoteli ya
Naura Spring, mjini hapa lilikuwa na upinzani mkali kutoka kwa washiriki wote
wa Redd’s Miss Tanzania.
Mbali na Magdalena warembo wengine waliofanikiwa kuingia
katika tano bora walikuwa ni Mary Chizi (Ilala), Irene Veda (Lindi), Belinda
Mbogo (Dodoma) na Sina Revocatus (Elimu ya Juu).
Akizungumza na Mtandao huu mjini hapa, Afisa Habari wa
Kamati ya Miss Tanzania, Haidan Ricco amesema warembo hao wataondoka kuelekea
Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es
Salaam.
Warembo wapatao 30 wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania,
ambalo kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji
chake cha Redd’s Original.
Chanzo Global Publisher.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA