Header Ads

Breaking News
recent

PETE ZA WATU MAARUFU DUNIANI NA THAMANI ZAKE

Asili Yetu Tanzania.Copyright

 Staa huyu "Hilary Duff" alivishwa pete ya ndoa na staa mwenzake "Mike Comrie" anayekamata dola milioni 1.25 kwa mwaka, na ilipofika wakati wa mwanadada huyu kuulizwa kidole chake cha mkono wa kushoto basi "Mike" aliitupia pete ya thamani ya dola milioni moja katika kidole cha staa huyu.

Hii ndio pete ya Diamond (alimasi) ambayo price William alipiga magoti mbele ya mkewe Kate Middleton na kuitupia katika kidole cha mwanadada huyu mrembo.Pete hii ya bei ghari duniani, ilikuwa ni ya hayati  "Princess Diana" ambaye ni mama yake na Prince William.

Mwana muziki mrembo duniani ambaye ana - make headline mpaka leo, yeye alivishwa pete ya uchumba na kinara maarufu wa muziki wa Hip hop Jay - z a.k.a Jigga miaka michache tu iliyopita, hata hivyo inasemekana pete hiyo inathamani ya dola milioni 5.

Wakati msanii Jermaine Dupri akimchumbia Janet Jackson mwaka 2004, mwanadada huyu alionekana kutupia pete, ingawaje Janet alikuwa akiwaambia waandishi wa habari kuwa wawili hawa ni wachumba lakini kufikia mwaka 2009 waliachana.

Mwanadada Halle Berry alikubali kuvalishwa pete ya alimasi na Eric Benet mnamo mwaka 2001.Hata hivyo ndoa hii haikudumu kwani waliachana miaka miwili tu baada ya kufunga pingu za maisha. Hivyo kufikia mwaka 2005 walipeana taraka rasmi. Na kwa sasa Berry ana binti yake wa aliyozaa na Gabriel Aubry.

 Brad Pitt kwa muda wa miaka saba na mpenzi wake Angelina Jolie ameamua kumvalisha pete iliyotengenezwa na madini ya Diamond/ alimasi, inayokadiliwa kuwa na thamani ya dola 500,000.

 Mwanadada Avril Lavigne aliwashangaza watu kutangaza kuvishwa pete ya uchumba mwezi Agost mwaka huu na Nickelback's Chad , pete hiyo ya alimasi inakadiliwa kuwa na thamani ya dola 350,000.

 Brian Austin alimuuliza mwanadada Megan Fox maswali yale yale ya sikuzote, mwanadada huyu alipojibu I DO, basi Brian alimtupia bonge la pete mwanadada huyu, yenye thamani ya dola milioni 80,000. Na baada ya muda mfupi tu, jamaa aliamua kumiliki mzigo kihalali kwa kufunga ndoa katika eneo lenye mchanga wa Hawaii.

 Maria Sharapova ni mwanamke mrembo duniani, ambaye alivalishwa pete kali na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa timu ya Lakers "Sasha Vujacic. Thamani ya pete hiyo ni dola 250,00. Mwana dada Sharapova alitupia utani kuwa....."Asante kwa mchumba wangu kuwa na ladha kubwa.

 Glamazon Khloe Kardashian aliibusu pete kwa mara ya kwanza, alipoulizwa swali letu lile na staa wa NBA Lamar Odom. Mchezaji huyu maarufu wa mpira wa kikapu katika timu ya Lakers alimvalisha staa huyu wa kike pete yenye thamani ya dola 850,000.

Mwanadada aliyejizolea umaarufu mkubwa duniani kwa miaka iliyopita Jenifer Lopez, ambae pia alisha wahi kuchukua tuzo kadhaa za mwanamke mrembo  duniani na kuandikwa katika gazeti maarufu la Fobes. J. Lo kuvalishwa pete kwake sii kitu kigeni saaana, kwani alishavalishwa na wanaume wa nne tofauti tofauti, ambaye miongoni mwao ni Ben Affleck ambaye alimvisha pete yenye thanani ya dola milioni 1.2, ukiachilia mbali ile ya Marc Anthony ambayo haikufua dafu.

Jessica Simpson alitupiwa pete kidoleni na Eric Johnson iliyotengenezwa kwa madini aina ya Ruby na Diamond iliyobuniwa na Neil Lane.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.