JAMBO FESTIVAL - NI TAMASHA LA VITU VYA ASILI LITAKALO FANYIKA OCTOBER 20-28, 2012 MKOANI ARUSHA.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
![]() |
|
Meneja mauzo na
masoko MEGA TRADE
INVESTMENT Gudluck Kway ambao ndio wadhamini wakuu wa
tamasha hilo.
|
Tamasha la vitu vya asili lijulikanalo kwa jina la Jambo
festival linatarajia kuanza kutimua vumbi oktoba 20-28jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa idea afrika
Augustino Namfua ambao ni waandaaji wa tamasha kubwa la jambo festival katika viwanja vya kijenge jijini Arusha
alisema kuwa maandalizi yote ya tamasha hilo yamekamilika na zaidi ya wadau 100
wamethibitisha kushiriki .
Alisema kuwa tamasha hili ni la kwanza kufanyika jijini hapa na linashirikisha vikundi
mbalimbali vya miziki ya asili pamoja ,
vyakula vya kiasili na ngoma.
Alisema kuwa katika
tamasha hilo kutakuwa na burudani mbalimbali ambapo siku ya kwanza ambayo ni
October 20 mchana kutakuwa na mdahalo
wa sanaa na utamaduni ambao utafanyikia via via,huku siku ya pili kukifanyika
maonyesha ya sanaa za mikono, siku ya tatu kutakuwa na chakula cha usiku
maalumu kwa wasanii wa sanaa za kiutamaduni ,siku ya nne kutakuwa na maonyesho
ya vyakula vya kiasili ambapo alisema kuwa kutakuwa na vyakula mbalimbali vya
makabila tofauti tofauti ambapo alisema
vitauzwa katika uwanja wa AICC kijenge.
Alisema kuwa lengo kuu la tamasha hili la jambo festival ni
pamoja na kuibua vipaji vya sanaa kwa vijana na pamoja na kuwaeleimisha vijana
jinsi ya kufanya shughuli za kijasiriamali pamoja na kujikinga na mgonjwa
mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.
Alitaja baadhi ya wathamini wa tamasha hili kuwa ni pamoja
na megatrade investment kupitia kinywaji chake cha k -vant gin,Coca Cola,Ujumbe
Ink,Arusha Hotel,Viavia restaurant,Mwandago investment,sundrise radio,Arusha
time,pamoja na Interlegence seccurty.
Kwa upande wa meneja meneja wa mauzo na masoko MEGA TRADE
INVESTMENT Gudluck Kwaya ambao ndio wathamini wakuu wa
tamasha hili kupitia kinywaji chao cha Kvant gin alisema kuwa kampuni yao
imeamua kuthamini tamasha hili kwakuwa ni tamasha linalodumisha utamaduni wetu
pamoja na kuenzi vyakula vyetu asili.
Alisema kuwa hii sio mara ya o ya kwanzakuthamini matamasha
bali walishathamini matamasha mbalimbali
na wao kama megatrade watandelea kuthamini pamoja na kusaidi jamii kwa
ujumla kama sera yao kampuni yao inavyosema.
Aidha alihaidi kuendelea kushirikiana na jamii katika
shughuli mbalimbali za maendeleo na kusema kuwa huu sio mwisho wao wa kuthamini
tamasha hili watakuwa wanathamini kila mwaka huku akisisitiza wananchi wa mkoa
wa Arusha kujitokeza katika tamasha hilio
Baadhi ya wasanii ambao watatumbuiza katika tamasha hili ni
pamoja na kikundi cha kuinua vipaji vya vijana wanaoishi katika mazingira
magumu kijulikanacho kwa jina la S.U.A.


No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA