Header Ads

Breaking News
recent

HIFADHI YA NGORONGORO NI KIVUTIO CHA ASILI KWA WAGENI WA NDANI NA WA NJE

Asili Yetu Tanzania.Copyright

OLDUVAI GORGE ni sehemu maarufu sana katika utalii wa ndani, sehemu hii ndipo fuvu la binadamu wa kwanza lilipogunduliwa miaka mingi iliyopita. Pichani ni sehemu ya udongo uliyokuwepo miaka mingi iliyopita, na hakuna mabadiliko ya ghafla yanayotokea katika sehemu hii, hivyo watanzania tupatapo nafasi, basi tutembelee eneo hili tutafurahi sana.
Vitu mbali mbali vya asili ni sehemu kubwa pia katika utalii wa ndani, na hapa ni mmoja wa waandishi wa habari akichagua vitu vya asili wakati wakiwa hifadhi ya Ngorongoro wiki hii.
Jamii ya wamasai ni sehemu pia ya kivutio kwa wageni watembeleao katika hifadhi zetu za Taifa, wao huangusha burudani ya asili ya ukweli.

Wageni wakiwa wanaangalia bidhaa zinazotengenezwa na wamasai zilizopo ndani ya hifadhi ya ngorongoro.

Hii ndio baiskeli ambayo inadaiwa mtafiti Dkt,Yoshiharu Sekino wa asili ya kijapani alitumia kutembelea nayo hadi Tanzania.

Story hii ni kwahisani ya Libeneke la Kazini.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.