Header Ads

Breaking News
recent

MAONYESHO YA SANAA YA VITU VYA ASILI YA 'SOBER HOUSE' ALLIANCE FRANCAISE YAZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM.

Asili Yetu Tanzania.Copyright


Kamishna kutoka Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw. Christopher Shekiondo akizindua rasmi maonyesho ya sanaa ya Sober House jijini Dar amesema kwa niaba ya tume ya kudhibiti dawa hizo Zanzibar na kwa Serikali kwa ujumla wanatambua mchango wa wadau mbalimbali uliosaidia vijana kuachana na tabia hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakukikisha asilimia kubwa ya vijana wanabadilika kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo sera madhubuti za Serikali na mipango mikakati ikiwemo utekelezaji wa Kampeni za ufahamu wa madhara ya madawa hayo.

Ameongeza kusema kuwa mikakati ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya inakabiliana na changamoto nyingi kutokana na uhaba wa vituo na wataalamu lakini Serikali haijakata tamaa na inaahidi kutimiza lengo hilo katika muda muafaka ikishirikiana na wadau mbalimbali na kuomba wadau wengine wajitokeze.

Mkurugenzi wa Chama cha maafisa Ustawi wa Jamii Bi. Anna Swai akionyesha Sanamu ya Msanii Mkongwe nchini Bi. Kidude iliyotengenezwa na mmoja wa vijana waliobadili muelekeo na kuamua kuachana na dawa za kulevya Zakaria Mwiru (kushoto) wakati wa ufunguzi wa kazi za sanaa.

Mgeni rasmi katika maonyesho ya Sanaa ya 'Sober House' yaliyozinduliwa jijini Dar es Salaam Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya visiwani Zanzibar Dkt. Shekiondo (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wadau wanaondesha mkakati wa kuwasaidia vijana kubadili tabia na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na badala yale kuonyesha vipaji walivyo navyo katika sanaa.

 Raia wa kigeni akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na vijana waliobadilika na kuamua kuacha tabia za utumiaji wa madawa ya Kulevya na kujishughulisha na sanaa.

 Mbunifu wa Mavazi nchini na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka a.k.a Kubwa la Maadui alikuwa ni miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.Pichani akipozi na moja ya mkoba uliosukwa na mkeka ikiwa ni kazi za vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya na kujifunza fani mbalimbali na mwishowe kuvionyesha kwa jamii.





No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.