Header Ads

Breaking News
recent

MSIKILIZE RICK ROSS ALICHOSEMA KABLA YA KUONDOKA KUHUSU WATANZANIA NA SHOO YA FIESTA 2012.

Asili Yetu Tanzania.Copyright

 Mtangazaji wa Choice Fm inayomilikiwa na Clouds Media Group, Vanessa Mdee akiwa wanafanya mahojiano msanii wa kimataifa kutoka Marekani, "Rick Ross" alikofikia katika hotel ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk, jijini Dar es salaam, huku mtangazaji kutoka Clouds Fm, Millard Ayo akirekodi mahojiano hayo. Rick Ross baada kuangusha shoo ya kali ya Serengeti Fiesta 2012 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam, ameweka historia katika shoo zote za Fiesta zilizokwisha kupita Tanzania.

Msanii Rick Ross pichani  na Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga  katika kutoa shukurani kwa kufanyika vyema tamasha la Serengeti Fiesta 2012 katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam Tanzania.

                     Msanii Rick Ross akiwa na Vanessa Mdee (kulia) na Feza Kessy (kushoto).

Rick Ross akipeana mkono na Millard Ayo mara baada ya mahojiano katika hotel ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk, dakika za mwisho mwisho msanii huyo kukwea pipa kurudi Marekani.

1 comment:

  1. Ilikuwa bonge la shoo, siku hiyo, pia big up Asili Yetu Tanzania.

    ReplyDelete

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.