MSANII THE GAME AMMWAGIA DISS ZA KUTOSHA JAY - Z KWA KUSABABISHA OBAMA KUTOFANYA VIZURI KATIKA MDAHALO ULIOPITA.
Asili Yetu Tanzania.Copyright
The West Coast rapper Game anazidi kuelekeza bunduki yake
yenye risasi za diss kwa Jigga na sasa amekuja kivingine akimtuhumu kwa
kusababisha Obama aperfom chini ya kiwango katika mdahalo uliopita.
Alipoulizwa mtazamo wake kwa performance ya Obama katika
mdahalo kwake ilikuwa ni kama alipewa gap la kumsema Jigga, Game aliunganisha
tukio la mdahalo wa Obama na Romney uliofanyika mapema mwezi huu na ushiriki wa
Jay-Z katika kampeni za Obama.
Alifunguka kwa kujiachia, “Nimeona mdahalo: maneno
hayakuwekwa poa saana, baadhi ya mada zilikuwa covered kwa usahihi.” Baada ya
hayo mawazo ya jumla, akafunguka zaidi “lakini alikuwa Obama. Inawezekana
alimsikiliza Jay-Z kabla ya kuingia pale he was a little bit in the zone and
couldn’t get it together. Lakini nampenda Obama ameshapata kura yangu.”
Baada ya hayo aliamua kuweka msisitizo alipokuwa anafanya
mahojiano na CBS Local “ngoja nikwambie kitu, Obama angeweza kuja na akasema
A-B-C zake katika hiyo debate na bado angepata kura yangu. Nampenda Obama,
ametulia na ana Swag na huyo ndiye rais wangu. Mitt Romney ni wa Republican. Na
siungani na chochote wanachokisimamia. Sio kama na diss imani ya mtu mwingine
yeyote na anachokipigia kura, lakini mimi nampenda Obama. And he can’t do no
wrong.” alimaliza Game.
Jay-Z ambae ni mtu wa karibu sana wa Obama kati ya
wanamuziki wa Marekani, hivi karibuni alihost tamasha la kumchangia Obama
katika kampeni zake na akatokea kwenye tangazo la kusapoti kampeni za Obama.
Jay- Z yuko mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa Barack
Obama anarudi White house na hata katika message ya matumaini aliyoiachia Obama
masaa kadhaa yaliyopita Jigga anaonekana kuifanyia kazi na kuakisi kile
alichosema Mr. president.
Obama amewapa nguvu wapiga kura kwa kujiweka katika nafasi
ya mpiga kura kisha akasema, “na mtaanza kuona nguvu ya kura zetu. Wakati rais
anaingia ofisini mwanzoni, kile alichokipresent kwa taifa ilikuwa ni matumaini.
Unajua, matumaini ya watu wote nchini ambao wangetazama na kujiona katika mambo
yanayowezekana…sasa watu wanatumia haki yao, na mtaanza kuona nguvu ya kura
zetu. . He made it mean something for the first time for a lot of people."
Mchakato wa kampeni unaendelea U.S.A lakini inaonekana
wanamuziki wengi wanamsapoti Obama hata kama wao wanabeef kati yao lakini
inapofikia hatua ya kumpigia kura Obama wanakuwa na maneno tofauti lakini
yanamaana moja tu “Obama again”.
No comments:
KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA