Header Ads

Breaking News
recent

AJALI YA BASI LILOKUWA LIMEBEBA WAJUMBE WA CCM MKOANI MWANZA, YAUWA.

Asili Yetu Tanzania.Copyright

Wanausalama barabarabani wakipima ajali hiyo iliyosababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ni dereva wa basi lenye namba za usajili T 853 BRB lililokuwa na wajumbe wa CCM kutoka wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza leo.

Wananchi wakishangaa ajali ya basi jinsi ilivyotokea.
BASI lililobeba wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutoka wilaya ya Kwimba limepata ajali na kuanguka eneo la Buhongwa wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza majira ya saa 3:30 - 4:00 asubuhi leo.
Imeelezwa kuwa dereva wa chombo hicho cha usafiri amefariki dunia papo hapo na wajumbe wengine saba kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando.
Chanzo cha ajali hiyo kinatajwa kuwa basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi lilikuwa katika harakati za kulikwepa lori aina ya Fusso ambalo lilikuwa likigeuza kujiweka sawa kuingia barabarani ndipo basi hilo lilipopoteza uelekeo na kulibamiza Fusso na kupinduka.
Wajumbe hao kutoka wilaya ya Kwimba, walikuwa wakiingia jijini Mwanza kwenye uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoa wa Mwanza unaofanyika leo uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.